Jeshi la Misri ladai kuua kimakosa

Image copyrightReutersImage captionKikosi maalum kimetumwa kuchunguza tukio la mauaji

Misri imesema jeshi lake la ulinzi limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imetuma kikosi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo

kwa upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na kusema kuwa ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa kina, Wizara ya mambo ya nje ya Mexico imethibitisha kuwa takriban raia wake wawili wameuawa na kuongeza kuwa inafanya jitihada kuwatambua waathirika wengine.
    tamko la wizara limesema , Balozi wa Mexico nchini Misri, Jorge Alvarez Fuentes alitembelea hospitali na kuzungumza na raia watano wa Mexico ambao hali zao zilikuwa njema.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company