Kubenea Amuumbua Dr. Slaa Mkutanoni,Kyela Mbeya

Hapa kuna video ya Kubenea akimchanachana Dr Slaa katika mkutano wa hadhara Kyela, Mbeya

Amesimulia sakata zima la Richmond kwa kudai kuwa wakati likiwakilishwa bungeni kulikuwa na ripoti mbili. Moja ya kumchafua Lowassa na ya pili ikidai Kikwete ndo mhusika wa Richmond
Amesema aliyekuwa akipinga ujio wa Lowassa Chadema ni Baregu na siyo Dr Slaa.
Amesema kamati kuu ya chadema ilijiridhisha kuwa Dr Slaa asingeweza kushinda uchaguzi wa mwaka huu kama angesimamishwa kuwa mgombea wa urais
Amedai kilichomponza Slaa ni mkewe ambaye alikuwa na uchu wa kuwa first lady
Baada ya hapo,Slaa alianza kampeni za kumpinga Lowassa ili ateuliwe yeye. Alimtuma Sugu aende Mbeya akawaambie waumini wa makanisa yote kuwa wao wanamtaka Slaa na sio Lowassa, lkn Sugu Alikataa.
Slaa pia alijaribu kumrubuni Tundu Lissu atangaze kumpinga Lowassa lakini naye alikataa pia na kujikuta akibaki peke yake, hali iliyomfanya ajivue uanachana
Amesema Slaa alikuwa Padri akaasi,alikuwa na mke akaasi, alikuwa CCM akajitoa, je ana principle gani za kuwashawishi watanzania wamuamini?
Dr Slaa ni msaliti na anatumia umaarufu wake vibaya
Slaa anadai kuwa nyaraka za Richmond alipewa na Mwakyembe, lakini ukweli ni kuwa mwakenye hawezi kuwa mtu sahihi wa kutoa nyaraka za Richmond kwa sababu wakati wa Ripoti hiyo, Mwakyembe alikuwa na kampuni yake ya kufua umeme ambayo alitaka ipite. Baada ya kukwama ndo akaanza ugomvi na Lowassa
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company