MBOWE: Ulofa na Upumbavu Wetu ni kwa sababu ya CCM

Mpekuzi blog
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ili umasikini unaowakabili Watanzania uweze kuondoka lazima washirikiane kuiondoa madarakani CCM.

Amesema ulofa na upumbavu wanaodaiwa kuwa nao Watanzania umesababishwa na Serikali ya CCM kwa kuwa haiwajali Watanzania.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora ambapo piaalilazimika kuwapigisha kura za mikono wananchi wa Nzega waliohudhuria mkutano huo ili kutatua mvutano wa wagombea wa ubunge katika Jimbo la Nzega Mjini lililokuwa na wagombea wawili wa Ukawa.

Wakati wa kura hizo, mgombea wa Chadema, Charles Mabura, aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Meza John.
Mgombea wa Ukawa alieteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Mabula (kulia) akipeana mkono na aliekuwa Mgombea wa nafasi hiyo kwa Jimbo la Nzega mjini, Mezza Leonard (kati) akiekubali kushindwa baada ya kupigwa kura ya wazi na wananchi wa Nzega Mjini, jana Septemba 6, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company