Wahamiaji:Ujerumani kudhibiti mpaka wake

Image copyrightReutersImage captionWahamiaji

Ujerumani inatarajiwa kuanzisha vidhibiti vya mda katika mpaka wake na taifa la Austria ili kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.

Awali msemaji wa kampuni moja ya reli kutoka Austria alisema kuwa treni zinazoelekea Ujerumani zimesitisha safari zake.Image captionNjia inayotumiwa na wahamiaji kuingia Ujerumani

Mjini Munich pekee,zaidi ya wahamiaji 13,000 waliwasili siku ya jumamosi.

Ujerumani inatarajia wahamiaji 800,000 kuwasili nchini humo mwaka huu.

Hatahivyo bwana Maiziere hakutoa maelezo kuhusu vile vidhibiti hivyo vya mpakani vitakavyofanya kazi.Image copyrightGettyImage captionUjerumani

Mwezi uliopita,alisema kuwa makubaliano ya usafiri wa viza ya Schengen ambayo huruhusu uhuru wa kutembea katika mataifa mengi ya Ulaya pia yatasimamishwa kwa mda.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company