Mwenyikiti Mstaafu wa Chama cha Wananchi Cuf, Prof Ibrahim Lipumba amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amekiuka sheria kwa kusitisha utangazaji wa matokeo kwani inaweza kuleta mgogoro wa kisiasa.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Azam Tv, Prof Lipumba amesema mwenyekiti wa ZEC alipaswa kuita majaji na wajumbe wa tume na kujadiliana na kuwatangaza walioshinda na lisichukuliwe kisiasa.
“Huwezi kufuta matokeo ya urais Zanzibar halafu useme uchaguzi wa Tanzania ni halali,”amesema Lipumba
Amesema katika katiba ya Zanzibar Ibara 28 (2) inasema rais atachia madaraka yake baada ya kumaliza miaka mitano na kuongeza kuwa mwenyekiti wa ZEC amedai kuwa kuhairishwa kwa matokeo ya urais kumesababishwa na kuwa na wapigakura wengi zaidi katika vituo kuliko wale walioandikishwa.
“Suala hilo walipaswa waulizwe wasimamizi na mawakala na kulalamika siku ile ya uchaguzi,”.alisema Lipumba
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago