HABARI KUU ZA LEO na OSCAR SAMBA
print this page
HABARI NA Oscar Samba
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

KITABU CHA WITO WA KITUMISHI. Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.

Ni Ujumbe uliopo kwenye hicho kitabu mada ya Mwisho inayoelekeza namna ya kuingia Shambani au kuanza huduma;

 Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa watumishi wengi wa leo, wanazitaka ishara na miujiza, pamoja na vitu vya mwilini kabla hawajaenda kuanza huduma.

Wanasahau maandiko husema kuwa ishara hizo zitaambatana na hao waaminio, ikiwa na maana kitu cha kwanza ni wao kuingia shambani, ndiposha ishara, na miujiza na mafanikio au vitendea kazi vya mwilini kama vyombo, majengo na hata mwanamke mjane wa sarepta hutokea kazini.

Siku moja wakati Roho ananifudisha jambo hili, alinipa mfano wa ajabu sana, aliniambia; Si unawaona madereva na magaria ya dalala, na makondakta wake, nami nilijibu ndiyo.

Ingekuwaje kama wangekaa nyumbani, au walipopaki magari yao, na kuanza kupiga debe wakiwa hapo, wangepata abiria?
Nalijibu hapana! Yenye alama ya mshangao, ndipo aliponiambia na watu wangu huwa katika mfano huo, wanapiga debe, ya kwamba gari lao linaelekea mahali fulani, lakini hawapo tayari kuliendesha na kuingia barabarani, yaani huanza kutafuta abiria, wakiwa au gari likiwa ndani, limeifadhiwa, bila kuliwasha na kuanza kazi barabarani.

Lakini madereva wa dunia hii, hulitoa gari lilipohifadhiwa wakiwa hawana abiria, ila wanapofika njiani au kituoni huanza kupiga debe na hatimaye kupata abiria, ikifika jioni, wana hesabu ya tajiri au ya gari, na wao wana riziki zao.

Watu wangu wasiowasha gari na kuanza kazi, nao ikifika jioni wanataka riziki zao, angali hawana hesabu ya tajiri, au ya gari.
Kwa hiyo hawana budi kuingia barabarani, maana huduma tayari nimeshawapa, ambayo ni gari. 

Mpendwa jambo hili ni kubwa, nalo ni pana, lina hitaji kulifahamu, maana ni kweli hata anayeuza duka, anapofungua asubui hajui atakayemuuzia, lakini wateja huja, na wewe huna budi kuanza huduma, wateja yaani washirika watakuja, na vitu kama vyombo, vya matangazo, na usafiri, vitakufuata tu.

Swali: Kuna abiria anayelipa nauli bila kuona gari? Sasa mbona wewe unataka vya mwilini bila kuingia shambani?
Kama Mungu akikujalia kukupa kabla, ni vyema, ila usimpangiye, ifanye kazi yake, kwa kutumia kipengele kile cha kuwa tayari kutumika popote, na ukumbuke Mwana wa Adamu hana pa kukilaza kichwa chake, ikiwa na maana ya kwamba, mazingira yoyote yasikuzuiliye kuifanya kazi ya Mungu.

Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya.
Biblia ya mafafnuzi, imetumia lugha nyepesi kidoko katika zitafutana;

(17Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu watatoa pepo na watasema
kwa lugha mpya.)

Ya Basic English imetumia neno ishara hizo zitakuwa nao hao wenye imani na jina langu;
(Mark 16:17 And these signs will be with those who have faith: in my name they will send out evil
spirits; and they will make use of new languages;)
Na ya King James Version, Imetumia neno, zitawafwata, maana yake, waende, alafu zije;

(17 And these signs shall follow them that believe; In my name shall they cast out devils; they shall speak with new tongues;)
Sasa chukua neno, Zita-wafwata, Zitakuwa nao, kuandana, na kufuatana, maana yake, ili kuvipata hivyo, unapaswa kwenda, navyo vije, usipofungua duka, na wateja wasipokuja, usilaumu wateja au muajiri wako, bali jilaumu wewe maana unapaswa kulifungua hilo duka, ndipo waone bidhaa, hakuna mtu ananunua mbuzi aliyepo kwenye gunia au kiroba, ni shariti aonekane kwanza.

Alafu pia hilo andiko linasema waaminio, au wanaoliamini jina la Yesu, nawe unapaswa kuwa na imani ya kwamba Yesu atakutokea tu, huko uendako, yupo kunguru atakayekutunza, wala usihofiye vya mwilini ya kwamba vitakuwaje.
Hakuna vyombo, hubiri bila vyombo, vitakuja tu, maana hata Yesu hakutembea na punda siku zote alizokuwa akiingia Yerusalemu, ila ipo siku aliingia na punda.

Sio kila mahali Yesu alihubiri juu ya jukwaa, ni mara chache sana alipata ofa za mitumbwi/boti na kuitumia kuingai ndani yake, na wakati mwingine alikuwa akikwepa makutano waliokuwa wakimsonga sana, pia na ili aweze kufikisha ujumbe vyema maana akiwa majini upepo wa mawimbi husafirisha sauti, nawe kuna siku utakutana na mtuimbwi wa wakina petro na kuupanda, yaani utapata jukwaa tu, wala usiwe na shaka.

KITABU KIKITOKA USIKIKOSE

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel  
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/ 
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/ 
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa 
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel  
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)
0 Toa maoni yako.

FAHAMU VIZURI KWA KUSOMA HAPA SIKU AMBAZO NI RAHISI KWA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO

jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile 
day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14. 

Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika suala zima la urefu wa MENSTRAL CYCLE, yaani 
idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia. Kundi kubwa la wanawake wana fall 
kwenye range ya siku 22-35. Japo walio-normal wana siku 28. Vile vile kuna wengine huwa na menstral 
cycle mbili, yaani fupi na ndefu. Hivyo walio na menstral cycle fupi, mathalani wale wenye siku 22, huwa 
vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu (period), yaani damu inaweza kukatika ndani ya 
siku 2 tu! Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) 
ambapo wengine huwachukua hata siku kati ya 5 hadi 8. 


Hivo basi, kama wewe ni mwanaume inakubidi umwelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo niliyoyasema 
hapo juu ili ikusaidie kui-pin point ile fertile day (yaani siku ya mimba). 


Swali: Je siku ya mimba ni ipi? 


Jibu lisilosahihi: Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile ya 14 baada 
ya dalili za kwanza za damu ya hedhi! Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 
14! Utaratibu huu ume-prove failure! Hii ni kwa sababu wanawake wana menstral cycle 
zinazotofautiana kwa urefu. Hivo basi jibu sahihi ni hili hapa chini: 


Jibu sahihi: 
1. Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ana menstral cycle ipi? Fupi au ndefu, ama zote mbili? 


2. Baada ya kujua urefu wa menstral cycle ya mwenzi wako then pin point siku ile ya mwisho halafu 
uhesabu backwards siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho. Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya 
mimba kwa mwanamke yeyote! 


Once you know the '15th day' from the last one, then you can manoeuvre whatever you want to get her 
pregnant or to avoid pregnancy! 

With this new approach of pin pointing the fertile day you will find that all women (menstral cycles) 
are covered, whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days! 


Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine: 

1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini: 
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd. 


Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba 
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day 
ndiyo siku anayoanza ku-bleed! 


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini: 


1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th. 


Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba 
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day 
ndiyo siku anayoanza ku-bleed! 


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini: 

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th. 


Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa 
mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo 
siku anayoanza ku-bleed! 


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO 
WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI: 

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama 
kawaida: 

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th. 


Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo 
siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke 
kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa 
kundi hili anaweza kupata mimba! 


Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo 
ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii 
anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku 
ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili 
linakuwa tayari kurutubishwa! 


Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa 
kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu 
kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa 
wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu! 


Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili 
suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao 
husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana 
ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo 
mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona 
wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine 
hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!
0 Toa maoni yako.

IMANI ZA KISHIRIKINA ZINAKWAMISHA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA





Na Amon Mtega Songea
BAADHI ya Wananchi Katika Kata ya Liganga Songea Vijijini Mkoani Ruvuma wamekuwa na Imani potofu wauguapo Maralia hivyo elimu ya Ugonjwa huo bado ni changamoto Vijjini.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Ernest Haule wakati akizungumza katika Siku yaZMaralia iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Shamba la Kahawa la Kampuni ya Aviv Tanzania LTD.

'Elimu ya Maralia Hapa ni changamoto na kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuandaa siku hii ya Maralia kwa kushirikiana na Kampuni ya Aviv katika Kata hii ya Liganga'anasema Mtendaji huyo na kuongezaMaralia ni Ugonjwa wa kawaida hivyo Wananchi wanapaswa wanapojisikia dalili za Maralia kuwahi kupima na kupatiwa matibabu badala ya kuamini ushirikina.

Kwa upande wake Msimamizi wa Shamba hilo la Kahawa kutoka Kampuni ya Aviv Tanzania LTD Amilt Kumar amesema kuwa wameandaa Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila Aprili 25 kwa Wafanyakazi 1000 Zkushindwa kufanya Shughuli zao sawasawa.
0 Toa maoni yako.

WANAUME CHANZO SARATANI YA MLANGO WA UZAZI

Na Hudugu Ng'amilo.
WANAUME wametajwa kuwa chanzo kikuu cha wanawake kupata ugonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi ambayo imekuwa tishio kwa sasa.

Mshauri wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la PSI-Tanzania, Dk. Mashafi Joseph, alieleza hayo jijini Dar es Salaam juzi alipozungumza na waandishi wa habari akizungumzia udhamini wao katika Jukwaa la Wanawake la 'Familia Kitchen Party Gala', litakalofanyika Aprili 27, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kupitia chapa yao ya familia.

Akifafanua hilo, Dk. Mashafi alisema kisayansi wanaume ndio wabebaji wa kirusi kinachosababisha ugonjwa huo kinachoitwa Human Papillomavirus (HPV) ambako kwao hakina madhara ila kinapofika kwa mwanamke ndipo anapata saratani hiyo ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

Kwa hapa nchini alisema saratani hiyo si tu inaongoza kwa vifo vya kina mama bali pia ni aina ya saratani ambayo inakuwa kwa kasi katika nchi za Afrika Mashariki huku Tanzania ikiwa na mzigo mkubwa wa wagonjwa.

Kuhusu udhamini wao kwa jukwaa la 'Familia Kitchen Party Gala', inayoandaliwa na Women Footprints Initiative, alisema wameamua kushirikiana nao kwa lengo la kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi.
CHANZO TANZANIA DAIMA
0 Toa maoni yako.

JUWA JINSI YA KUZUIA WATU WASIFUNGUE AKAUNTI YAKO YA FB AU EMAIL HATA KAMA WANA PASSWORD YAKO

Kuna wakati hata kama mtu anayo PASSWORD yako ya FB au akaunti yako ya barua pepe bado hawezi kuingia kwa akaunti yako.
Unaweza dhibiti watu wengine wasifungue akaunti yako ya email au Facebook kwa kufuata huduma ya ku sign in mara mbili.
Yaani ipo hivi:
1. Mara ya kwanza una sign in kama kawaida kwa kutumia ID na PASSWORD yako, ambapo hivi ndio umekuwa ukifanya wakati wote.
Ila kwa huduma hii ya kusign mara mbili, ID na PASSWORD pekee hazikuruhusu kuingia kwa akaunti yako.
2. Utakapomaliza ku sign in , utatakiwa kufuata hatua ya kuweka CODE maalum ambayo utatumiwa kwa njia ya ujumbe mfupi kwa simu yako. Au la pengine tayari ulipojiandikisha kwa huduma hiiya kusign mara mbili, basi uliweza ku download CODES maalum ambazo ni wewe tuu ndio utaweza kuzitumia.
---Fuata maelekezo ya jinsi ya kutumia huduma hii ya kusign mara mbili kwa kubofya link hapo chini.

HUDUMA YA FACEBOOK KUSIGN IN MARA MBILI ...BONYEZA HAPA

HUDUMA YA GMAIL KUSIGN IN MARA MBILI ........BOFYA HAPA

HUDUMA YA YAHOO KUSIGN IN MARA MBILI .......BOFYA HAPA
0 Toa maoni yako.
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company