WILAYA YA KYELA – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBANDA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. POLISI WALIWAKAMATA WATU WATANO RAIA WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI AMBAO NI {1}.ALAKEZA S/O MOSE,MIAKA 32 {2}. BULALAHUBWA S/O KALODATI, MIAKA 25 {3}. ALAKAZYA S/O ALINI, MIAKA 6 {4}. NISHUNA D/O DORINA, MIAKA 6, NA {5}. MUNYEZE D/O JOZINA, MIAKA 9 . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUKUTWA KATIKA KANISA LA BABTISTI KIJIJINI HAPO WAKIOMBA HIFADHI. WATUHUMIWA WAMEKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU.
WILAYA YA MBOZI – KUSALIMISHWA KWA SILAHA MOJA AINA YA GOBOLE
MNAMO TAREHE 23.01.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WALISALIMISHA /TELEKEZA BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE YENYE NAMBA – TOWKK 340. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUTELEKEZA SILAHA HIYO JIRANI NA KITUO KIDOGO CHA POLISI IYULA NA POLISI KUICHUKUA . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA KWA KUTOA TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI /TENGENEZA SILAHA BILA KIBALI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATAHADHARISHA WAMILIKI/WATENGENEZAJI HARAMU WA SILAHA HIZO KUZISALIMISHA HARAKA INGAWA MUDA WA “OFFER” UMEMALIZIKA KULIKO KUSUBIRI KUKAMATWA.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 24.01.2013 MAJIRA YA SAA 18:56HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NZIGWA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.MAKENZA S/O IGEMBE, MIAKA 45, MSUKUMA, MKULIMA NA 2. MILEMBE D/O MALA,MIAKA 65,MSUKUMA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NZIGWA WAKIWA WANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI . WATUHUMIWA NI WAKULIMA NA WAUZAJI WA BHANGI. BHANGI YOTE IMETEKETEZWA KWA KUCHOMWA MOTO SHAMBANI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WAMILIKI NA MAHALI YALIPO MASHAMBA YA BHANGI KUZITOA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YA WAHUSIKA ZICHUKULIWE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.