Kenya yapitisha sheria ya kuoa wake wengi

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepitisha sheria ambayo itawaruhusu wanaume nchini humo kuoa idadi waitakayo ya wanawake pamoja na kuwepo ukosoaji mkubwa wa makundi ya wanawake na makanisa.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais wa Kenya imesema Rais Kenyatta ametia saini muswada wa Sheria ya Ndoa ya Mwaka 2014 ambayo inajumuisha ndoa mbalimbali zikiwemo za Kiislamu, Kihindu na Kikristo. Kwa mujibu wa sheria hiyo ndoa ni baina ya mwanamke na mwanamme ambao wanafunga ndoa kwa khiari. Aidha sheria hiyo inasema mwanamme anaweza kuoa mke mwingine pasina kupata idhini ya mke au wake alio nao.

Baraza la Kitaifa la Makanisha Kenya NCCK limepinga vikali sheria hiyo. Aidha Jumuiya ya Mawakili Wanawake Kenya FIDA imesema itawasilisha pingamizi la kisheria dhidi ya muswada huo. Nchini Kenya sawa na aghalabu ya nchi nyingine za Afrika, kuoa wake wengi ni jambo la kawaida miongoni mwa makabila mbalimbali na katika jamii za Waislamu. Wengi wanasema sheria hiyo inatambua uhakika ambao upo tayari kwani kuna idadi kubwa ya ndoa za wake wengi. Mbunge Junnet Mohammad amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema, “Wakati mwanamke wa Kiafrika anapoolewa, anapaswa kujua kuwa mke wa pili yuko njiani na wa tatu…hii ndio Afrika."
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company