Habari kutoka Brazil zinasema bwawa la maji lililoko karibu na eneo la kuchimba chuma kusini mashariki mwa Brazil mkoani Minas Gerais limebomoka, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 15.
Bwawa hilo linaloendeshwa na kampuni ya Samacro lilibomoka jioni na kusababisha maji na matope kuingia mji wa Bento Rodrigues wenye wakazi 620 ulioko umbali wa kilomita saba kutoka kwenye bwawa.
Ofisa wa ulinzi wa jamii wa Mariana Bw Braz Azevedo amesema hali ya sasa ni mbaya, na uchunguzi umeanza, sambamba na juhudi za uokoaji.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago