Majina yanaweza kubuniwa kutoka kwa vipande vya lugha tofauti, kubadilisha maneo kwa mfano kutoka nyuma ukirudi mwanzo na kadhalika. Kwa mfano neno bata unaweza kuwasikia vijana wakenya wakisema taba na kuoga wanasema kugao.
Nimeanza na maelezo hayo kuonyesha namna lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihuni na baadhi ya wasomi wa Kiswahili inatofautiana kutokana na mtu anachosema na mahali anaposemea.
Hata hivyo kwa wataalamu wa isimu jamii ( social linguists) watakupiga mawe ukikashifu matumizi ya sheng. Wengine hata wamefanyia utafiti kipengee hicho.
Ingawa kuna mvutano mkubwa kuhusu matumizi ya sheng ama lugha simo, ni muhimu kutaja kuwa kuna baadhi ya maneno yaliyoanza kama sheng na yakaswahilishwa.
Kwa mfano nchini Kenya, Matatu ni magari ya uchukuzi wa umma ama matwana kwa Kiswahili sanifu. Vivyo hivyo, Tanzania chombo hicho kinaitwa daladala ambalo si jina la Kiswahili sanifu lakini limetiwa katika matumizi.
Hata hivyo kuna hasara kubwa ya kutumia baadhi ya majina ya sheng ambayo yanapotosha maana halisi ya maneno hayo ya Kiswahili.
Kwa mfano nchini Rwanda mtu akiwa hajakamilika kwa namna moja au nyingine watu wanamuita kasorobo. Kwa hakika kasorobo ni neno la Kiswahili kumaanisha kuna upungufu wa robo ya kitu kujalizia mahali fulani kama vile dakika kumi na tano za saa na kadhalika.
Hivyo inapotumika katika mazungumzo inawakanganya waswahili. Si hayo tu, Burundi ndio kuna mambo, eti muasi kwa lugha simo ya huko ni msichana mrembo.
Kwa Kiswahili sanifu muasi ni mwanamgambo ama mtu msumbufu tu asiyeambilika wala kusemezeka.
Kenya na Tanzania ni nchi ambazo zinajulikana pia kuibuka na misimo mbalimbali na inayopotosha maana halisi ya maneno ya Kiswahili. Nchini Tanzania nilimsikia mtangazaji mmoja akisema msichana mrembo anaitwa Mkwaju. Tunavyojua katika Kiswahili mkwaju ni namna moja ya kiboko cha kumchapa mtu. Je sasa twabadilisha jina la mrembo kuwa kiboko? Mambo mawili kando kabisa. Tanzani amtu atakwambia anasikia ubao kumaanisha kuwa anaona njaa. Inavyoeleweka ni kuwa ubao ni sehemu ya mti ama mbao katika Kiswahili sanifu. Na huko Tanzania mtu anapokwambia patachimbika ana maana ya kuwa pameharibika jambo. Utata unaojitokeza hapa ni kuwa patachimbika ni kitenzi cha Kiswahili kumaanisha hali ya pengine kufanya shimo mahali ama kutoboa kitu ilhali kuharibika ni kusambatarika kwa hali ama kitu fulani. Hizo ni dhana mbili tofauti kabisa kama mbingu na ardhi.
Nchini Kenya pia mambo ya sheng yanapigiwa upatu sana hususan na vijana. Hata hivyo ni muhimu kutaja kuwa matumizi ya maneno fulani huvuruga Kiswahili Kabisa. Kwa mfano katika lugha simo Kuro ni kahaba lakini ukweli ni kuwa katika Kiswahili kuro ni mnyama wa porini wa jamii ya paa anyefanana na kulungu. Yaani hapa kosa la kwanza ni kumlinganisha binadamu na mnyama. Pili neno mbuyu Kenya lina maana ya baba lakini katika Kiswahili ni mti unaozaa mibuyu na ikiwekwa semi na iwe "kuzunguka mbuyu" basi inamaanisha kutoa hongo.
Kadhalika neno demu ambalo linatumika Tanzania, Kenya na Jamhuri ya demokrasia ya Congo lina maana ya msichana lakini katika Kiswahili sanifu ni kitambaa kinachofunika mwanamke maziwa anapolima ama tambara hivi. Je unapomwita msichana demu hujui kwa Kiswahili unamlinganisha msichana huyo natambara labda? Je huo ni uungwana? Kenya watu wanasema masa ni mama katika lugha simo lakini katika Kiswahili sanifu masa ni matendo mabaya yanayofanywa na mtu.
·
Athari nyingine ya lugha simo ni kuwa inaweza
kuwafanya watu waache kuyatumia maneno mengine ya Kiswahili wakidhania ni
Sheng. Baadhi ya maneno hayo ni kama vile manzi ambalo ni neno la Kiswahili
sanifu kumaanisha msichana ila wengi hulitumia kama
sheng. Ashara kumaanisha idadi kumi ni sawa kwa Kiswahili lakini Kenya
watu wandhania hiyo ni sheng.
I
Mara ya mwisho imebadilishwa: 18
Juni, 2009 - Imetolewa 14:34 GMT
|
|
|
|
|
|
|
|
Matamshi
|
MTAMSHI KATIKA LUGHA.
Hili ni muhimu kabisa katika kazi ya utangazaji. Hapa
tunazungumzia unavyoweza kutamka kwa |
|||
|
MTAMSHI KATIKA LUGHA.
Hili ni muhimu kabisa katika kazi ya utangazaji. Hapa
tunazungumzia unavyoweza kutamka kwa ufasaha maneno hasa ikizingatiwa BBC
inaaminika na wasikilizaji wake tangu zamani kuwa ina weledi wa lugha ya
Kiswahili.
Haipendezi na utaonekana kichekesho ukichanganya L na R na
hili la siku hizi linalowapa taabu kubwa vijana la H na A. Ama watu nane badala
ya watu wanane.
Ni nzuri na si nzuli, habari na si abari. Wapo wanaotamka
mathalan watu nane wameuawa .....Kiswahili hakikubali hilo, bali unachotakiwa kutamka ama kuandika
ni watu wanane.
Jee ikiwa kwa idadi ya watu wawili ukikatisha kama ilivyo kwa nane utatamkaje? ni watu mbili! Hapana ni
watu wawili.
Neno jingine linalowasumbua waandishi kuliandika na
kulitamka ni dharura, wapo wanaoliandika na kulitamka dharula ni makosa kutumia
dharula ila ni dharura. Hili ni muhimu kabisa.
Lugha ya Mtandao
Kwa sasa matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC yanapatikana
kupitia mtandao wetu http://www.bbcswahili.com.
Hapa unaweza kusoma yale ya muhimu tunayotangaza kila siku
na kila mara huwa tunabadilisha yaliyomo kadri tukio linavyobadilika.
Kinachohitajika hapa ni kuandika kwa lugha nyepesi zaidi
itakayomfanya msomaji asome kwa uelewa wa hali ya juu na kwenda kwenye kile
kinachotakiwa na sio kuandika ki-gazeti. Kumbuka kuzingatia yanayohitajika
katika kutafsiri. Hakuhitajiki lugha ya kuzungukazunguka. Sarufi
|
|
UMAKINI WA LUHA YA KISWAHILI KWA WATANGAZAJI.
Unapotangaza kwa lugha ya Kiswahili unatakiwa uwe na uelewa wa sarufi ya lugha yenyewe. Ni muhimu kupangilia kwa ufasaha sentensi zako kwa unayoyatangaza.
Unapotangaza kwa lugha ya Kiswahili unatakiwa uwe na uelewa wa sarufi ya lugha yenyewe. Ni muhimu kupangilia kwa ufasaha sentensi zako kwa unayoyatangaza.
Jitahidi kupangilia unachokusudia kukieleza kwa ufasaha wa
kisarufi. Kwa mfano nchi hizo zote mbili zitakuwa na mazungumzo ya pamoja.
Hapa nchi kawaida haziwezi kuzungumza ila kwa Kiswahili
sahihi ni viongozi wa nchi hizo mbili watakutana ama watafanya mazungumzo.
Kutafsiri lugha
|
|
Uadilifu wa lugha
|
|
Uadilifu wa lugha ni jambo muhimu kwa unayoyatangaza. Jaribu kadri uwezavyo kuepuka matamshi na maneno ya mitaani yanayoweza kukifanya unachokitangaza kionekane ni mzaha.
Hapa tunasisitiza matumizi ya maneno sahihi wakati wa
kutangaza. Mathalan si vyema mtangazaji kutumbukiza neno ambalo hata mwenyewe
unayetangaza linakufanya usite kulitamka kwa vile maana yake inakuletea
ukakasi.
Ni vyema ukajizoeza kutumia neno upungufu badala ya lile
linalochomoza zaidi siku hizi mapungufu. Neno upungufu halina wingi. Tunapotaja
idadi ya watu hatusemi watu ishirini na nne au watu kumi na mbili.
Kiswahili kinasisitiza hapa useme watu ishirini na wanne au
watu kumi na wawili. Linapokuja suala la tarehe katika Kiswahili hatusemi
tarehe moja au tarehe mbili.
Kiswahili safi
na kinachopendeza tumia tarehe mosi ama tarehe pili. BBC Idhaa ya Kiswahili
inazingatia hilo
katika matangazo yake.
UTAFSIRI
Moja ya kazi inayofanywa katika chombo changu cha habari ni kutafsiri kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili. Ukifahamu Kifaransa, Kijerumani ama Kiarabu utakuwa na utajiri mkubwa wa kufanya kazi ya kutafsiri kuwa nzuri zaidi.
Moja ya kazi inayofanywa katika chombo changu cha habari ni kutafsiri kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili. Ukifahamu Kifaransa, Kijerumani ama Kiarabu utakuwa na utajiri mkubwa wa kufanya kazi ya kutafsiri kuwa nzuri zaidi.
Ili ueleweke vyema kile
unachotafsiri ni vizuri ukielewe unachotafsiri kabla ya kuanza kuandika. Hii
itakuondolea shida ya kutafsiri neno kwa neno hali itakayofanya kazi yako ya
kutafsiri isieleweke.
Mathalan neno concern inategemea sentensi. Ukikuta
imeandikwa It does not concern you, kwa kiswahili chepesi ni haikuhusu. Lakini
neno hilo hilo
likitumika kwa sentensi hii. His poor health concerns us, tafsiri yake
ni afya yake mbaya sana
inatupa wasiwasi.
Halikadhalika unapokutana na sentensi kama hii mathalan, The
Government of Zimbabwe has
welcomed the call...hapa tafsiri yake usiandike serikali ya Zimbabwe imekaribisha wito...bali tafsiri yake
ni Serikali ya Zimbabwe
imeafiki au imekubaliana na wito...
Ufupisho wa maneno
Hapa nasisitiza ufupisho wa maandiko hasa mashirika
mbalimbali. Mathalan WHO hili ni Shirika la Afya Duniani, WFP ni Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani, FAO Shirika la Chakula Duniani, nakadhalika.
Lakini kwa vile utaweza kukutana na maneno haya na mengine
yanayofanana, ni vyema ukauliza namna yanavyoandikwa kwa kirefu badala ya
kukurupuka.