Sababu za upungufu wa mbegu za kiume


Matunda husaidia kuongeza mbegu za uzazi. 
  
HALI ya maisha pamoja na mazingira husika yanayomzunguka binadamu imeelezwa kuwa ni chanzo cha kushuka kwa nguvu za kiume.
Madaktari  wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni  gazeti la The Independent llilopo nchini Uingereza  liliripoti kuwa hali ya afya ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.
Utafiti huo ulionyesha kuwa katika miaka ya 1989 hadi 2005  ulionyesha kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi robo tatu yake walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka  1989 na  2005, kwa mujibu wa gazeti moja la Uingereza lilisema kwamba  “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikisababisha nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za ndani ambazo zinabana, pia wataalamu  walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu ya nguvu hizo kushuka bado haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya  hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na daktari mmoja maarufu katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo aliyejulikana  kwa jina la Solomon Wasike ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa mwenye tatizo kama hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo alikuwa na umri wa mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya kupima juu ya uwezo wake wa kuzaa.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa baada ya maelezo hayo aliamua  kuchukua mbegu zake mwanaume huyo  kwa ajili ya vipimo aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo iliyosababisha mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa kiume wenye matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba vijana wengi wanaokuja katika hospitali  hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na jambo hili linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaokuja ni vijana.
Aliongeza kuwa hali hiyo inafanya tuamini kuwa licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa lakini asilimia kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya  hali ya maisha wanayopitia pamoja na mazingira wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa bado hazijafanywa  juu ya tatizo licha ya kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume kutoka katika katika hospitali mbalimbali.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company