EPAImage captionRais wa Urusi, Vladmir Putin
Rais wa Urusi,Vladmir Putin ametoa wito wa kuwepo kwa mpango wa kikanda wa kupambana na wanamgambo wa Islamic State.
Putin amemuhakikishia kumuunga mkono Rais wa Syria, Bashar al-Assad,ambaye mataifa ya magharibi na upinzani nchini Syria wamemtaka aondoke madarakani.
Mzozo wa Syria unatarajiwa kuwa miongoni mwa ajenda zinazotazamwa kwa karibu zaidi wakati Viongozi wa dunia wanapokutana katika mkutano wa Umoja wa Mataifa,jijini New York nchini Marekani.
Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron anatarajiwa kulegeza msimamo wake dhidi ya Assad katika hotuba yake wiki hii.
Cameron sambamba na Rais wa Marekani, Barrack Obama na rais wa Ufaransa, Francois Hollande walikuwa wakimtaka rais Assad aondolewe madarakani ili kuleta amani Syria, msimamo ambao umekuwa ukipingwa na Putin.
Kukutana kwa viongozi wa Ulaya kunazidisha wito wa kuwepo kwa msukumo wa kidiplomasia nchini Syria wakati huu ambapo kumekuwepo na wimbi la wakimbizi wanaoelekea Ulaya.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago