Rais Barack Obama akihutubia kwenye mkutano wa maendeleo endelevu 2015 katika Umoja wa Mataifa
Rais wa Marekani Barack Obama alisema dunia ina kazi zaidi ya kufanya pale linapokuja suala la kutokomeza umaskini uliokithiri duniani kote. “Hivi sasa wanaume, wanawake na watoto wapatao milioni 800 wanajitahidi kuishi kwa chini ya dola 1.25 kwa siku. Fikiria hilo. Wanataabika huku wakiwa hawana kitu tumboni,” alisema Obama. Saa kadhaa baada ya kuwasili mjini New York City siku ya Jumapili kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Marekani aliisihi dunia kuchukua hatua wakati wa kufunga kikao cha mkutano wa maendeleo endelevu.“Tunaweza kujisifia katika kile tulichokamilisha, lakini hatuwezi kupumzika, Obama alisema. “Wakati wavulana na wasichana 11 wanakufa kila dakika kutokana na sababu zinazozuilika, tunajua tunakazi zaidi ya kufanya”.
Baadhi ya viongozi wa dunia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa
Viongozi wa dunia walikutana kuidhinisha malengo 17 ya maendeleo endelevu-SDGs, ikiwemo kumaliza umaskini, kufanikisha usawa wa jinsia na kulinda bahari pamoja na maeneo ya mazingira ya viumbe hai na visivyo hai, pembeni ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Juhudi za ulimwengu zinajengwa katika Malengo ya Maendeleo ya Millenium-MDG yaliyoanzishwa mwaka 2000 na mwaka 2015 kama mwaka uliolengwa, miongoni mwa mambo mengine, kupunguza kwa nusu viwango vya umaskini uliokithiri, kuzuia kusambaa kwa HIV na ukimwi, na kuongeza kiwango cha usawa wa jinsia katika uandikishaji kwenye shule za msingi.
Rais Barack Obama akihutubia katika Umoja wa Mataifa huko New York City
Katika matamshi yake Jumapili, Rais Obama alielezea “mafanikio ya kihistoria” ya juhudi za miaka 15 za MDGs ambazo zililenga juu ya matarajio ya malengo manane. “Kwa sababu dunia imekutana pamoja katika juhudi zisizitarajiwa, viwango vya njaa ulimwenguni tayari vimepunguzwa. Mamilioni ya wavulana na wasichana hii leo wapo shule,” Obama alisema. “Kuzuia na matibabu ya surua na malaria na kifua kikuu yameokoa takribani maisha ya watu milioni 60”.
Umoja wa Mataifa ulisema kwamba tangu mwaka 1990 idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri imeshuka kwa zaidi ya moja na nusu kutoka watu bilioni 1.9 mwaka 1990 hadi watu 836 milioni kwa mwaka 2015.
Umoja wa Mataifa pia ulielezea kuwa takwimu za vifo vya watoto zinaonyesha kuwa watoto wanaofariki kabla ya kufikia umri wa miaka mitano vimeshuka kwa zaidi ya moja na nusu.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago