MAJIRA YA
KUTEMBELEWA NA MUNGU
Naam kwa
tabasamu mwanana lifananalo na lile lililomkuba BWANA yetu YESU KRISTO pale
msalabani mara pazia la Mbinguni lilipo pasuka na Kunene yote yamekwisha; na
kukaribisha katika mkala hii tamu na mwanana ewe mteule wa Ufalume wa Mbinguni.
Katiak siku
ya leu muhimu kwetu na ufalume wa mbinguni siku ya PASAKA ambayo tuaminio
katika KWELI ile KUU ni siku ya kuamdhimisha kufufuka kwa BWANA yetu YESU
MNAZARETHI.Ujumbe huu ummetolewa masaa machache yaliyopita katika kanisa la
Kiroho lililopo hapa mkoni Arusha eneo la Morombo kanisa la VICTORY CHRISTIAN
CENTRE T.A.G (VCC) na mwangalizi mkuu
katika eneo hili la makanisa ya T.A.G.
Makala yetu
ya leo inalenga kukuabarisha majira ya
kujiliwa kwetu na MUNGU wetu,Msingi mkuu wa neno tunaupata katika kitabu
cha Luka 19 -41 tunaona pale Yesu
anazungumzana na jiji la Yerusalemu kwa kutokutambua majira ya kujiliwa kwake.
Mungu
anasema ya kwamba haya ni majira ya kujiliwa kwa kanisa lake sasa na haitakuwa
kama Yerusalemu ambayo haikutambua ila wewe utatambua.
Utakuwa kama
watu wawili ambao walitambua akiwemo
Zakayo na Batimay o katika Marko 10.
Katika ijuma
kuu wafu walifufuka, miamba ilipasuka wanathailojia wanaamini ya kwamba watu
hawa walienedelea kutembea mijini hadi pale Yesu alipofufuka na kwenda nae
katika Yerusalemu mpya.
MAANA NA MAKUSUDI YA
KUJILIWA NA MUNGU.
KUTEMBELEWA
NA MUNGU; ni kipindi maalumu katika wakati ambacho Mungu humjilia mtu na
kumtembelea mtu binafsi au kikundi cha watu kama kanisa au familia,kabila ,ukoo
au Taifa na Mungu hufanya hivyo kwa kusudi maalumu.
Mungu
huchaguwa mwenyewe katika kalenda yake,kwahiyo wewe mwenyewe kama mtu binafsi
huweza kutembelewa na Mungu au familia yako.
Mungu alokusudi maalumu
lakukutembelea.
KUSUDI LAKE
Yapo mambo
makuu matano ambayo ningalipenda kukujuza siku ya leo amayo huwakilisha
makusudi haya mema ya MUNGU kwetu.
1.Ili kuwa na ushirika nasi,mwanzo 3:8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini wakati wa jua
kupunga.Mungu alihitaji kutengeneza au kuimarisha ushirika na watu
wake.Mungu akitembea na wewe katika ulimwengu huu atafanya mapito yako kuwa
mepesi na kufanya maisha yako yasiwe ya kawaida.
Ona mzee
kama Zakayo anapanda juu ya mtii,nae alifanya jambo ambalo sio lakawaida Ufunuo
wa Yohana sura ya 3,ukisoma utaelewa zaidi.Kumbuka kitabu hiki ni kwa ajili ya
watu wanaomjua yeye ndio maana kinaitwa Ufunuo,kumbuka katika kkujiliwa kwako Baraka
ya kwanza ni Mungu kuwa na ushirika na wewe.
2.Ili kutukomboa katika hali na
mazingira ambayo huleta mateso,kama yale ya wana wa Iziraeli kule Misri,Kutoka 3:7-8 Bwana akasema hakika nimeyaona mateso ya
watu wangu walioko misri, name nimekisikiaa kilio chao kwa sababu yya
wasimamizi wao; maana na yajuua aumivu yao 8 nami nimeshuka iliniwaokowe na
mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka katika nchi ile hata nchi njema kisha
pana;nchi ijaayo maziwa na asali hata mahali pa Mkanani ,na Mhiti na Mwashori
na Mperizi na Mhivi na Myebusu.
Sisi sote
katika maisha ya Kikirito yatupasa tupietie katika majaribu,imani yetu
inapojaribiwa Mungu hutuwezesha kupita,fahamu ya kwamba majaribu sio kituo cha
kudumu bali ni kituo cha Muda na haikukusudiwa kuwa sehemu ya kudumu kwahiyo
usikubali kukata tamaa.
Ingawaje
jaribu huweza kudumu kwa muda mrefu ila sio la milele na jaribu hilo linapokuwa
ni la muda mrefu maranyingi hugeuka na kuwa mateso ila usikubali kukata tamaa
kwani Mungu amejianda kukutembelea kama alivyo mhaidi Ibrahimu ya kwamba watu
wako watakaa katika nchi ya ugeni miaka mia 400 lakini nitawatoa.
Mungu anayajua
maumivu yako pia anayajua mateso yako tabu ambazo mtu hawezi kuyaona yeye
anayajua ndio maana ameweka wakati wake wakukujilia na ukifika nayang’oa kama
gr’eda.
3.Ili kutupiganiia. Joshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua
lipokua karibu na mji wa Yeriko akavua
macho yake na kuangalia na tazama mtu
mume akasimama mbele yake naye alikuwa na upanga wazi mkoni mwake ; Yoshua akaamwendeeaa
na kumwambiaa Je! Wewe huu upandde wetu au upndde wa adui zzetu?
Ukiendelea
utaona jinsi ambavyo Mungu aliutana nae na hakua adui wala jitu baya.Yoshua katika
mazingira haya alikuwa akikabiliana na majaribu na mapamabano makubwa mno,mji
waliokuwa wakikabiliana nao ulikuwa na ulinzi mkubwa sana ila Mungu hakumwacha.
Mung
alimwamnia Yoshua awe na moyo mkuu awe na moyo wa ujasiri nawe usiogope,Jifunze
ili ushicheke na mtu anaetaka kukuangamiza,mtu anaetafuta hatima yako,usikubali
kucheka nae na MUNGU wa Yoshua
atakupigania ondoa hofu.
Kwa mamala
ya jina la YESU nakutangazia ya kwamba vita hivyo sio vyako bali ni vya BWANA,kumbuuka
Mungu hujitokeza ili atupiganie.
4.Kuburudishwa. Matendo ya Mitume 3:19 Tubuni basii
ili nije zipate nayakti za kuburudishwa kwa kuwepo kwake BWANA. Baada ya mapito
ni mapumziko.
Hata wacheza
mpira huwa na muda wa mapumko,Mungu ameweka majira ya kutupooza, ya kutufuta
jasho,ni wakati wakunyamazisha maadui zako,huku ukipata wakati wakuburudishwa.Kuna
mambo makuu matatu hapa;
(a)
Mungu
huleta uamsho na kuleta au kurejesha tumaini na furaha yako ya awali.
(b)
Waebrania
4:1,6 Mungu hapa huleta pumziko,ipo siku inakuja ambapo chakula haitakuwa
mgogoro,,utaanza kufikiria juu ya mafuta ya gari au sehemu ya kujenga.
(c)
Nyakati
za urejesho,Mungu hurejesha vilivyo potea, 1samweli
30:18-19 Utasoma na kuona Daudi
alivyokuta ameibiwa ,ila Mungu wa Daud atakurejeshea vilivyo potea ya mkini
ni,mali au watoto.Kama alivyo mrejshea Ayubu nawe wakati wako waja,Miaka iliyoliwa
na nzike itafidiwa;amina. Soma zaidi hapa Ayubu 42:10.
5.Mungu hututembellea ili kutujulisha
hatima yetu,2samwli 7:1 Utaona; Bada ya Mungu kumpa
amani Daudi kwa kumshindia madui zake Daudi alitafakari jinsi ya kumjengea
Mungu nyumba,pia utaona jinsi Mungu alivyokuja kusema dhidi ya hatima ya maisha
yake miongoni mwa hayo alikwepo Sulemani,Mungu alifanya nae ahadi ilikuja kumtoa
mtawala wa milele ambae ni Yesu Kristo.Zaidi
unaweza kusoma, Yohana 21,Matendo 29.
MUNGU HUTUTEMBELEA ILI
UTUONESHA HATUA ZA MAISHA.
Tafadhali kwa mwendelezo
wa makala hii usiache kututembelea leo alasiri ili upate mwendelezo wa habari
hii NJEMA,,nakutakia PASKA NJEMA na MUNGU wangu AKUTANE NA HAJA YA MOYO WAKO; Amina.