Uganda yamkamata mfungwa wa zamani wa Guantanamo Bay

Wanajeshi wa UPDF na vikosi vya polisi Uganda wakifanya doria mtaani mjini kampala, July 3, 2014 baada ya kutolewa onyo la uwezekano wa kutokea shambulizi

Serikali ya Uganda imemtia nguvuni mtu mmoja ambaye aliwahi kushikiliwa katika gereza la Guantanamo Bay la nchini Cuba kwa tuhuma kuwa huenda alihusika katika mauaji ya mwezi uliopita ya mwendesha mashitaka aliyekuwa akisimamia kesi za ugaidi nchini Uganda.
Ripoti ya mwandishi wetu Kennes Bwire wa Kampala, Uganda

Jamal Abdullahi Kiyemba alikamatwa pamoja na watu wengine watatu wakati wakifanya mkutano nje kidogo ya mji wa Kampala hapo Jumanne, kulingana na Fred Enanga, msemaji wa polisi.

Enanga alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano na maafisa wa Marekani. Kiyemba aliwahi kuishi Uingereza na baadae alisafiri kwenda Pakistan ambako alikamatwa kama mtuhumiwa wa ugaidi na baadae kupelekwa Guantanamo Bay mwaka 2002. Aliachiliwa mwaka 2006 na kurejeshwa Uganda baada ya kukataliwa kuingia Uingereza.

Polisi wa Uganda Jumanne waliwakamata watu wengine kadha kuhusiana na mauaji ya mwendesha mashitaka Joan Kagezi yaliyofanyika hapo Machi 30, mwaka 2015 ambapo inaaminika alilengwa na magaidi kwa vile alikuwa akiendesha kesi kadha za kigaidi nchini humo.

Ulinzi umekuwa wa hali ya juu nchini Uganda hasa mjini Kampala tangu ubalozi wa Marekani kutoa ilani ya mashambulizi ya kigaidi mwezi uliopita na baadaye kuuawa kwa Kagezi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company