CHUO CHA UANDISHI WA
HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA
RASIMU YA KATIBA YA
WANAFUNZI
2014
YALIYOMO
Ibara Kichwa cha
habari
SURA YA KWANZA
SERIKALI YA WANAFUNZI,BUNGE,SPIKA
WA BUNGE,UTAWALA MKUU WA CHUO NA BARAZA LA KATIBA NA SHERIA.
SEHEMU YA KWANZA.
1.VIONGOZI WA WANAFUNZI……………………………………………………………………………………….
2.BUNGE LA WANAFUNZI NA SPIKA WA
BUNGE…………………………………………………………………........................................
3.BARAZA LA SHERIA NA KATIBA…………………………………………………………………………………........................
SEHEMU YA PILI
4.UTAWALA MKUU WA CHUO………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA TATU
5.RAIS WA SERIKALI YA
WANAFUNZI……………………………………………………………………………………………..
6.MAKAMO WA RAIS WA SERIKALI YA
WANAFUNZI………………………………………………………………………
7.AFISA UHUSIANO WA SERIKALI YA
WANAFUNZI……………………………………………………….
8.KATIBU WA SERIKALI YA WANAFUNZI………………………………………………………………………
SURA TA PILI.
BARAZA LA
MAWAZIRI,HAKI,MLEZI WA WANAFUNZI,ELIMU, HABARI,NIDHAMU,SHERIA NA UTAWALA BORA.
SEHEMU YA KWANZA
9.BARAZA LA MAWAZIRI……………………………………………………………………………………………
10.HAKI ZA WANAFUNZI…………………………………………………………………………………………………
11.MLEZI WA WANAFUNZI…………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA PILI
12.ELIMU………………………………………………………………………………………………………………………..
13.HABARI…………………………………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA TATU.
14.NIDHAMU……………………………………………………………………………………………………………………….
15.SHERIA, KATIBA NA UTAWALA BORA………………………………………………………………………………..
SURA YA TATU.
MICHEZO, BURUDANI,AFYA,
MAKAZI.
SURA YA KWANZA
16.MICHEZO NA BURUDANI………………………………………………………………………………………….
17.AFYA NA MAKAZI. ……………………………………………………………………………………………………..
SURA YA NNE.
MAADILI YA
WANAFUNZI,VIONGOZI, WALIMU NA WAJIBU.
SEHEMU YA KWANZA
18.MAADILI YA WANAFUNZI………………………………………………………………………………………….
19.MAADILI YA WALIMU KWA WANAFUNZI. …………………………………………………………………………
20.MAADILI KWA VIONGOZI WA WANAFUNZI.
……………………………………………………………………
SEHEMU YA PILI
21.WAJIBU WA MWANAFUNZI. …………………………………………………………………………………….
22.WAJIBU WA MWALIMU KWA MWANAFUNZI ……………………………………………………………………
SURA YA TANO
ULEZI WA
DARASA,UCHAGUZI NA UDHIBITI WA MATUMIZA MABAYA YA FEDHA.
SEHEM YA KWANZA
23. MWALIMU WA DARASA ……………………………………………………………………………………………
24.WAWAKILISHI WA DARASA …………………………………………………………………………………………
SEHEMU YA PILI.
25.TUME HURU YA UCHAGUZI YA WANAFUNZI
WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA
UTANGAZAJI ARUSHA…..……………………………………………………………………
SEHEMU YA TATU
26.MKAGUZI WA HESABU NA MATUMIZI YA
FEDHA ZA VIONGOZI WA WANAFUNZI…………
UTANGULIZI.
Kwa hiyari
yetu sisi wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha,tumeamua kuwa na katiba hii ambayo
itakuwa ndio msingi mkuu wa sheria na kanuni katika maisha yetu hapa chuoni.
Dhumuni la
katiba hii ni kudumisha amani,haki na kutimiza madhumuni na shabaha pamoja na
maono yanayotufanya tuwepo hapa chuoni.
SURA YA KWANZA
SERIKALI YA WANAFUNZI,BUNGE,SPIKA
WA BUNGE,UTAWALA MKUU WA CHUO NA BARAZA LA KATIBA NA SHERIA.
SEHEMU YA KWANZA.
1.VIONGOZI WA
WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa
na viongozi wa wanafunzi watakao gawanyika katika nguzo kuu tatu,nguzo hizo ni;
(a)
Serikali
ya wanafunzi,nguzo hii itakuwa chini ya kiongozi mkuu ambaye ni Rais wa
serikali ya wanafunzi,jukumu lake kubwa ni kuwaongoza wanafunzi.
(aa)Viongozi wengine waliopo katika nguzo hii ni; Makamu wa Rais
wa serikali ya wanafunzi, Katibu wa serikali ya wanafunzi, Afisa uhusiano wa
serikali ya wanafunzi, baraza la mawaziri,Idara/kamati za serikali ya wanafunzi
kwenye vitengo mbalimbali na Wawakilishi wa darasa.
(b)
Nguzo
ya pili ni Bunge,nguzo hii itakuwa chini ya kiongozi mkuu ambaye ni spika wa
bunge.Jukumu lake kubwa ni kutunga
sheria na kuisimamia serikali.
(c)
Nguzo
ya tatu ni baraza la sheria na katiba,nguzo hii ipo chini ya kiongozi mkuu
mwenye cheo cha mwenyekiti kiongozi, jukumu kubwa la baraza hili ni kutafsiri
sheria
2.BUNGE LA WANAFUNZI NA
SPIKA WA BUNGE.
(1).Kutakuwa
na bunge la wanafunzi litakaloongozwa na spika wa bunge.Pia wabunge wake
watachaguliwa na wanafunzi kwa utaratibu uliopo kwenye ibara ya 25 (6)
(a)
Kuwaondoa
viongozi walioshindwa kutekeleza wajibu wao madarakani akiwemo Rais,
(b)
Kutunga
sheria,
(c)
Kujadili
na kupitisha sera,kanuni na mipango ya serikali ya wanafunzi,
(d)
Kusimamia
idara zilizopo chini yeke,
(e)
Kuisimamia
na kiushauri serikali ya wanafunzi,
(f)
Kuidhinisha
au kutokuridhia uteuzi wa baadhi ya viongozi,
(g)
Kuikosoa
na kufuatilia mwenendo na utendaji wa serikali ya wanafunzi.
(3)Majukumu
ya Bunge yanaweza kuongezeka kulingana na kanuni zake.
(4)Bunge
litapaswa kutengeneza kanuni ambazo zitaunda muundo mzima wa uongozi wa bunge
na jinsi ambavyo litafanya shughuli zake.
(5)Kama
bunge litapoteza imani na Raisi,Makamu wa Raisi, Afisa uhusiano au Katibu wa serikali ya wanafunzi, litalazimika
kufuata Utaratibu ufuatao ili kumondoa madarakani;
(a)
Hatua
ya kwanza,lazima kuwe na sababu za msingi, sababu hizo zweza kuwa;
(aa)Kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa muda wa siku sitini
mfululizo kutokana na uzembe,
(bb)Kuugua ugonjwa wa akili,
(cc)Kuugua maradhi yoyote ambayo yanamzuia kutekeleza wajibu
wake kwa muda wa siku sitini mfululizo,
(dd)Kukiuka misingi ya uongozi, sheria na katiba ,maadili ya
uongozi na uanafunzi,
(ee)Kufanya kosa kubwa lililosababisha kupewa adhabu ya kusimamishwa
masomo kwa zaidi ya kipindi cha muda wa siku thelathini, ila kosa na adhabu
hiyo lazima vithibitishwe na baraza la
sheria na katiba ya kwamba ni halali .
(b)
Bunge
litajadili sababu husika na kupiga kura ya kutokuwa na imani na kiongozi huyo.
(c)
Kama
idadi kubwa ya kura itaonesha kutokuwa na imani na kiongozi huyo,tume ya
uchaguzi itapaswa kuchukua hatua ikiwemo kusitisha uchaguzi wa nafasi hiyo kwa kufuata
taratibu husika.
(6) Spika wa bunge ndiye atakayekuwa kiongozi mkuu wa shughuli
zote za bunge.
3.BARAZA LA SHERIA NA
KATIBA.
(1)Kutakuwa
na baraza la sheria na katiba.
(2) Baraza
hili litagawanyika katika ngazi kuu mbili ambazo ni ngazi ya juu na ngazi ya
chini ya maamuzi.
(3) Muundo wa uongozi wa ngazi ya juu.
(a)
Ngazi
hii itakuwa na viongozi wakuu watatu na wajumbe wengine wane.
(b)
Kiongozi
mkuu wa ngazi hii atakuwa na cheo cha Mwenyekiti kiongozi.
(c)
Msaidizi
wake atakuwa ni makamu mwenyekiti.
(d)
Pia kiongozi mwingine atakuwa ni katibu wa
baraza hili.
(e)
Wajumbe
hao wanne watachaguliwa na viongozi hawa watatu kwa sifa na vigezo
vitakavyowekwa na bunge.
(f)
Viongozi
hawa wakuu watatu watachaguliwa na bunge kwa sifa na vigezo watakavyoviweka ambavyo lazima vihusishe uwezo na upeo wao wa kisheria pamoja na
uadilifu wao.
(g)
Wanapaswa
kuhakikisha ngazi ya chini inatimiza wajibu wake au wao au kuutekeleza kutokana
na sababu mbalimbali pale wanaposhindwa kufanya hivyo.
(h)
Pia
wanapaswa kupitia maamuzi yote ya kiutendaji yanayofanywa na ngazi ya chini.
(i)
Bila
kuathiri masharti yoyote ya katiba hii na sheria nyinginezo , viongozi hawa
hawatawajibika kwa bunge wala kuondolewa madarakani na bunge ila kama wanafunzi watakosa imani na kiongozi
au baraza zima watapaswa kupiga kura ya kutokuwa na imani aidha na baraa zima
au kiongozi husika.Kura hiyo itasimamiwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na
Utangazaji Arusha .
(4) Majukumu ya ngazi ya juu.
(a)
Ngazi
ya juu itahusika na rufaa kutoka ngazi ya chini Ufafanuzi wa kisheria pamoja na
hukumu.
(b)
Wanapaswa
kusikiliza kesi zenye kuhitaji maamuzi makubwa ikiwemo;
(aa) Utata katika
hukumu au maamuzi ya Kufukuzwa chuo kwa mwanafunzi
(bb)Kusimamishwa masomo kwa mwanafunzi au adhabu ya wiki
mbili mfululizo,
(cc)Maamuzi ya Bunge yenye utata, serikali au utawala wa juu
wa chuo.
(5)Viongozi
wa ngazi hii ndio watakokuwa viongozi wakuu wa baraza hili.
(6) Kwa utashi au kulingana na ukubwa wa tatizo ngazi
ya chini inaweza kupeleka shauri au tatizo lolote kwenye
ngazi hii ya juu ambapo bila kujadili uamuzi huu,ngazi hii itapaswa kulifanyia
kazi.
(7) Ngazi
hii ya chini ya maamuzi itahusisha viongozi watakaoteuliwa na Rais na kupitishwa
na baraza la mawaziri.-
(a)
Viongozi
hawa watakuwa watatu na wataitwa wanadhimu,kiongozi wao ataitwa mnadhimu mkuu.
(b)
Ngazi
hii itahusika na ufafanuzi wa sheria na utafsri wa sheria, pia makosa madogo
yenye kuhitaji adhabu ndogo.
(c)
Ngazi
hii inapaswa kuhakikisha ya kwamba serikali inatunga kanuni kwa kupitia wizara
zake, ambazo zitakuwa za haki,na zenye kukidhi mahitajio.
(8) Maamuzi
yoyote yatakayochukuliwa na baraza hili la sheria na katiba lazima yahusishe usikilizwaji
wa pande zote mbili yaani mlalamikiwa na mlalamikaji.
(9) Ngazi ya
juu ya baraza hili halitakuwa na uhalali wa kutoa maamuzi bila kuwa na kikao rasmi
kitakachohusisha wajumbe zaidi ya wawili na viongozi wawili kati au wote watatu
wakuu.
(10) Ngazi ya chini inaweza kutoa maamuzi bia
kikao na maamuzi hayo yanaweza kufanywa na mnadhimu mmoja bila kumshirikisha
mwingine kama kuna sababu ya msingi.
(11) Maamuzi yote yatakayokuchuliwa na ngazi
ya juu ya baraza hili lazima yawe ni kwa mujibu wa katiba hii,sheria au kanuni
halali.Pia ngazi ya chini ya maamuzi itapaswa kutoa maamuzi kwa vigezo hivyo ila hekima,desturi
na busara zinaweza kutumika katika maamuzi yao lakini katika kutoa adhabu ndogo
na sio katika kuongeza adhabu.Kipengele hiki hakiwapi mamlaka viongozi wa ngazi
ya chini kuvunja kipengele chochote cha katiba hii,sheria kanuni wala taratibu
zozote zile halali.
(12)Kama
mtuhumiwa hataridhika na maamuzi kutoka kwenye ngazi ya juu ya baraza hili anapaswa
kupeleka malalamiko yake kwa mlezi wa wanafunzi ambaye atapaswa kuyapitia na
akiona yana mantiki atakutana na baraza la sheria na katiba ili shauri hilo
lipitiwe upya.
(13)Kabla ya
kutoa hukumu wajumbe watakutana na kukubaliana katika maamuzi,kama wajumbe
watatofautiana maamuzi watapaswa kukaa kwa pamoja wajumbe wanaokubalina
kimaamuzi na kuandaa hukumu.Mara baada ya hatua hiyo kila pande itasomo maamuzi
yao mbele ya mlalamikaji na mlalamikiwa na upande utakaoungwa mkono na wajumbe
wengi kwa kura mbele ya mlalamikaji na mlalamikiwa ndio utakaoshinda.
SEHEMU YA PILI
4.UTAWALA MKUU WA CHUO.
(1).Katiba
hii inatambua uwepo wa utawala mkuu wa chuo ambao kiongozi wake mkuu ni
mkurugenzi wa mafunzo wa chuo hiki cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.Pia unahusisha wakufunzi wote wa chuo hiki
pamoja na idara zake.
(a)
Utawala
huu unafanya kazi kwa mujibu wa katiba waliyonayo na katiba hii ya wanafunzi.
(2)Ufuatao
ni wajibu wake kwa wanafunzi;
a)
Kuheshimu,kutii
na kuilinda katiba hii ya wanafunzi wa cho cha Uandishi wa Habari na Utangazaji
Arusha,pia sheria,kanuni na taratibu
halali zilizowekwa na wanafunzi, serikali ya wanafunzi,bunge au baraza la
sheria na katiba.
b)
Unawajibu
wa kufuatilia mwenendo wa wanafunzi na vyombo vyao vyote vya uongozi.
c)
Unapaswa
kuhakikisha unatimiza malengo na dhamira ya wanafunzi kuwepo chuoni hapa na
kutoa haki zao za msingi kama ilivyo kwenye mitaala,taratibu za NACTE au wizara
yenye dhamana husika ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,katiba,sheria au
taratibu pia kama ilivyoainishwa kwenye fomu ya kujiunga na chuo.
d)
Hautakuwa
na mamlaka yoyote ile ya kuivunja serikali ya wanafunzi,bunge, baraza la sheria
na katiba wala kushinikiza kujiuzulu au
Kusimamishwa madaraka kwa kiongozi
yeyote wa wanafunzi bila kufuata Utaratibu uliopo kwenye 4(3).
(3) Kama
kiongozi yeyote wa utawala wa juu wa chuo ,serikali ya wanafunzi au mwanafunzi
yeyote au darasa litapoteza imani na kiongozi
yeyote wa ngazi yoyote wa wanafunzi aidha kweye serikali,bunge au baraza
la katiba; hanabudi kufuata utaratibu ufuatao:
(a)Watapaswa kupeleka malalmiko yao kwa Afisa uhusiano wa
serikali ya wanafunzi au mlezi wa serikali ya wanafunzi.
(b)
Mlezi
wa wanafunzi au Afisa uhusiano wa
wanafunzi wakiyaona malalamiko hayo ni ya msingi watapaswa kuyapeleka kwenye
ngazi zifuatazo;
(aa)Kama malalamiko hayo yanamhusu waziri au baraza lake, watapaswa kuyapeleka
kwa Rais wa wanafunzi ili achukue maamuzi stahiki mara baada ya kuyatafakari
kwa kina.
(bb) Kama malalamiko
hayo yatamhusu kiongozi yeyote wa idara au kamati yoyote ile basi watayapeleka
kwenye wizara yenye dhamana husika ili wizara hiyo ichukue maamuzi stahiki,
(cc)Kama malalamiko hayo yanamhusu Kiongozi wa idrara ya
ukaguzi wa hesabu za fedha na matumizi ya
wanafunzi,au mbunge,Afisa uhusiano,Makamu wa Rais,Katibu wa wanafunzi au Spika
wa bunge.
(dd)Kama malalamiko
hayo yanalihusu Bunge, basi malalamiko hayo yatapelekwa kwa spika wa bunge ,
bunge litayajadili na kuyachukulia hatua stahiki.
(ee)Kama malalamiko hayo yatamhusu kiongozi wa darasa,basi Afisa
uhusiano au mlezi wa wanafunzi atapaswa
kushirikiana na wizara ya elimu na kuyafikisha kwa darasa husika ili wachukue
maamuzi stahiki.
(ff)Kama malalmiko hayo yatamhusu Raisi basi yatapaswa
kupelekwa kwa spika wa bunge na bunge litafuata Utaratibu uliowekwa kwenye
ibara 2 (5)
SEHEMU YA TATU
5.RAIS WA SERIKALI YA
WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa
na Rais wa serekali ya wanafunzi wa chuo
cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha, atakayechaguliwa na wanafunzi kwa
mujibu wa matakwa ya katiba hii ya chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha
(2).Rais ndyie
kiongozi mkuu wa ngazi zote kwa serikali ya wanafunzi.
(3).Yafuatayo
ni majukumu ya Rais.
(a)
Kuteua
baraza la mawaziri na pia kulivunja punde litakapokiuka misingi na taratibu
zautendaji kazi.
(b)
Kuvunja Bunge la wanafunzi siku kumi na tano
kabla ya kuanza zoezi la uchaguzi mkuu au punde litakapokiuka misingi yake ya
utawala
(c)
Ni
mshauri wa wanafunzi na walimu dhidi ya wanafunzi.
(d)
Kusimamia
na kufuatilia utekelezaji wa wajibu wa wanafunzi na utimizwaji wa haki zao.
(e)
Anapaswa
kutekeleza wajibu wake kama mwenyekiti katika vikao vyote vya baraza la
mawaziri, vikao vingine muhimu na baraza
la wanafunzi.
(f)
Ndiye
mwenye maamuzi ya mwisho katika serikali ya wanafunzi.
6.MAKAMU WA RAIS WA
SERIKLI YA WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa
na makamu wa Rais; atahitajika
kupendekezwa na Rais na kugombea nae kama mgombea mwenza wakati wa uchaguzi, na
punde atakapoondoka madarakani Rais atamteua makamu mwingine.
(2)Majukumu
yake;
a)
Ndiye
mshauri na msaidizi mkuu wa Rais,
b)
Atapaswa
kutekeleza majukumu na kuchukua mamlaka ya Rais wakati Rais akiwa nje ya ofisi.
c)
Atapaswa
kukaimu nafasi ya Urais endapo Rais;
(aa).Atafariki,
(bb).Atajiuzulu
(cc).Ataugua mfululizo kwa zaidi ya miezi miwili.
(dd).au Ataondolewa na Bunge.
(cc)Kusimamishwa masomo.
(3)Makamu wa
Rais atakaimu nafasi hiyo kwa kipindi chote ambacho tume itakuwa ikiandaa
utaratibu wa uchaguzi mdogo au mkuu kwa ajili ya nafasi hiyo. Kipindi hiki
hakitapaswa kuzidi siku kumi na nne.
(d) Atapaswa kuwa mjumbe kwenye kikao cha baraza la mawaziri.
(e) Atashirikiana na Rais kiushauri katika uteuzi na muundo
wa baraza la mawaziri.
(f) Atapaswa kusikiliza na kutekeleza shughuli zote atakazoagizwa
na Rais.
(4) Bila
kuathiri masharti yoyote ya katiba hii makamu wa Rais hatakuwa na uwezo wa kuchukua
majukumu mazito ya Rais wakati Rais akiwa nje ya ofisi kwa kipindi chochote bila
kupata kibali cha Rais .Majukumu hayo yaweza kuwa;
a)
Kulivunja
baraza la mawaziri au ,
b)
Kulivunja Bunge
7.AFISA UHUSIANO WA
SERIKALI YA WANAFUNZI
(1).Kutakuwa
na afisa uhusiano wa wanafunzi, atachaguliwa na wanafunzi kupitia utaratibu
uliowekwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha
(2).Majukumu
yake.
a)
Ndiye
msemaji mkuu wa wanafunzi na serikali yao.
b)
Anajukumu
la kudumisha au kutengeneza mahusiano mazuri kati ya walimu na wanafunzi,
c)
Anapaswa kutetea haki,maslahi ya wanafunzi na kufuatilia
uwajibikaji wa wanafunzi pia walimu
dhidi ya wanafunzi.
d)
Atapaswa kuhudhuria vikao vya baraza la
mawaziri kama mjumbe.
e)
Atafanya
kazi kwa kushirikiana na mlezi wa wanafunzi.
f)
Anapaswa
kusikiliza malalamiko,ushauri kutoka kwa wanafunzi au walimu dhidi ya wanafunzi
na kuyatatua/kuyafanyia kazi au kuyafikisha sehemu husika.
g)
Atakuwa
na jukumu la kutengeneza na kujenga taswira safi dhidi ya wanafunzi/chuo pia
atakuwa na jukumu la kusafisha taswira ya wanafunzi au serikali yao.
8.KATIBU WA SERIKALI YA
WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa
na katibu wa serikali ya wanafunzi, atakayechaguliwa na wanafunzi kupitia
utaratibu uliowekwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(2).Yafuatayo
ni majukumu yake;
a)
Katibu
huyu ndiye atakayekuwa mratibu wa shughuli zote za kila siku za serikali ya
wanafunzi.
b)
Atapaswa
kupeleka ripoti zote,shughuli na maazimio ya Bunge la wanafunzi na baraza la
mawaziri pia uwajibikaji, na ufanisi wa kila wizara au waziri mmoja mmoja kwa Rais wa serikali ya wanafunzi.
c)
Atakuwa
msimamizi wa shughuli zote za kiserikali bungeni ambapo atashiriki kama waziri.
d)
Atapaswa
kumshauri Rais kuhusu utendaji na uwajibikaji
wa waziri/wizara au kiongozi yeyote aliepo katika nguzo ya serikali.
e)
Atapaswa
kutekeleza majukumu na shughuli atakazoagizwa na Rais au makamu wake.
f)
Atapaswa
kuandaa vikao vyote vya baraza la mawaziri au vikao vingine halali na kuhifadhi
kumbukumbu ya maazimio au maudhui ya vikao hivyo,
g)
Ndiye
msimamizi wa vikao hivyokiratiba na kiajenda ,
h)
Bila
kuathiri mashariti yeyote ya katiba hii, katibu hataingilia majukumu ya Rais
kwenye vikao hivyo; Kwani Rais ndiye
mwenyekiti na msemaji mkuu wa vikao
hivyo.
SURA TA PILI.
BARAZA LA
MAWAZIRI,HAKI,MLEZI WA WANAFUNZI,ELIMU, HABARI,NIDHAMU,SHERIA NA UTAWALA BORA.
SEHEMU YA KWANZA
9.BARAZA LA MAWAZIRI.
(1).Kutakuwa
na baraza la mawaziri litakaloteuliwa na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo
cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(2).Sifa za
mawaziri.
(a)
Achaguliwe kutokana na uwezo alionao kwenye wizara
husika.
(b)
Awe
na uwezo wa kuyamudu majukumu ya wizara husika.
(c)
Aridhie
nafasi hiyo.
(d)
Asiwe
na wadhifa wowote baada ya kuchaguliwa kwenye
serikali ya wanafunzi,bunge, baraza la sheria na katiba wala tume ya
uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(3).Majukumu
ya mawaziri.
(a)
Kusimamia
idara/kamati zote zilizopo chini yao.
(b)
Mawaziri/waziri
anapaswa kutekeleza wajibu na shughuli zake zote kama alivyoagizwa na Raisi,makamu wa Rais au katibu pia kwa mujibu
wa kanuni,taratibu,sheria au katiba zote mbili yaani ya utawala wa juu wa chuo
au katiba hii ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(c)
Kutengeneza
kanuni au sera za serikali kwa kupitia utaratibu utakaopangwa na bunge.
(d)
Mawaziri
watapaswa kuiwakilisha serikali bungeni kwa kupitia majukumu yao ya kiwizara
(aa)Mawaziri wakiwa bungeni hawatahesabika
kama wabunge na hawatakuwa na haki yoyote ya kibunge badala yake watahitajika
kutolea maswala ufafanuzi baada ya kupata kibali kutoka kwa spika wa bunge.
(bb) Mawaziri hawa wakiwa bungeni
wataketi sehemu tofauti na wabunge pamoja na katibu wa serikali ya wanafunzi.
(cc)Waziri akihitaji kutolea swala ufafanuzi kwa utashi wake pasipo
kuhitajika kufanya hivyo na wabunge kupitia spika wa bunge, atapaswa kupeleka
ombi kwa katibu wa serikali ya wanafunzi atakayepaswa kulipeleka kwa spika wa
bunge ambaye ndiye mwenye wajibu wakutoa kibali.
(4).Adhabu
itatolewa kwa waziri au kiongozi mwingine yeyote atakayetoa siri halali ya
baraza la mawaziri,serikali au kikao chochote halali; Adhabu hizo zaweza kuwa,
(a)
Kusimamishwa uongozi,
(b)
Kufukuzwa
uongozi au
(c)
Adhabu
yoyote halali na stahiki.
10.HAKI ZA WANAFUNZI.
(1).Kila
mwanafunzi anayo haki ya kuthaminiwa kwa imani yake ya kidini.
(2).Ni haki
ya wanafunzi kupata majibu na ufafanuzi wa maoni yao au maswali yaliyopo kwenye sanduku la maoni kwenye
baraza la chuo.
(3).Sanduku
la maoni litapaswa kukaa kwenye mazingira rafiki kwa wanafunzi.
(4).Ni haki
ya mwanafunzi kusikilizwa,uhuru wa kutoa maoni yake na kupata majibu sahihi
kutoka kwenye mamlaka husika.
(5).Ni haki
ya mwanafunzi kupata muongozo wa ratiba kuhusu mambo yote muhimu kwa muda watakaokuwepo
chuoni kutoka kwa mamlaka husika.
(6). Ni haki
ya mwanafunzi kupata ruhusa ya kuahirisha masomo yake kwa muda pale atakapokuwa
na sababu au tatizo la msingi,yaweza kuwa;
(a)
Ujauzito (b) Ajali (c) Ukosefu wa ada/fedha (d)
Maradhi (e) Au sababu zozote zenye uzito
mkubwa.
(7).
Mwanafunzi atakayerejea ataendelea na muhula aliouwacha pia hakutakuwa na
malipo ya ziada kama hapo awali alishalipia muhula huo.
(8).Ni haki
ya mwanafunzi kusoma/kufundishwa masomo yote kama ilivyo kwenye Utaratibu wa
chuo au mtaala.
(9). Ni haki
ya mwanafunzi kupata vifaa kutoka kwenye mamlaka husika kwa ajili ya elimu ya
vitendo.
(10).Bila kuadhiri
kipengele chochote cha katiba hii au ya utawala wa juu wa chuo wala kanuni yoyote au sheria, mwanafunzi
atakefanya kosa nje ya eneo la chuo na ikabainika hakulifanya kama mwanafunzi
wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji
Arusha na wala hakuwa kwenye
masomo ya vitendo; mwanafunzi huyo hatahukumiwa kama mwanafunzi wa chuo.
11.MLEZI WA WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa
na mlezi wa wanafunzi atakayeteuliwa na utawala mkuu wa chuo.
(2)Kama wanafunzi watapoteza imani naye, basi
watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa katibu wa serikali ya wanafunzi atakayepaswa
kuyapeleka kwa spika wa bunge ili bunge
lijadili na kisha kupiga kura ya kutokuwa au kuwa na imani naye.
a)
Kama
bunge litakosa imani naye basi katibu wa serikali ya wanafunzi atapaswa
kufikishiwa taarifa hiyo kwa utawala mkuu wa chuo ili wachukue hatua
stahiki.Utawala huu unaweza kufuta uteuzi wake na kumteua mwingine au kubariki
uteuzi wake hali itakayo mfanya aendele na wadhifa huo.
(3) Zifuatazo
ni sifa za mlezi wa wanafunzi.
(a)
Awe
ni mwalimu katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(b)
Awe
na uelewa wa kutosha kuhusu wanafunzi.
(c)
Awe
amefundisha katika chuo hiki zaidi ya siku sitini.
(d)
Pia
awe tayari kuifanya kazi hii.
(4) Majukumu
ya Mlezi wa serikali ya wanafunzi;
(a)
Anawajibika
kama mshauri na mlezi mkuu wa wanafunzi,serikali ya wanafunzi, bunge na baraza
la sheria na katiba.
(b)
Atapaswa
kusikiliza na kutatua matatizo yote ya wanafunzi kabla ya kwenda katika ngazi
ya juu ya utawala.
(c)
Atapaswa
kuhakiki maamuzi yote yaliyofanywa na ,serikali ya wanafunzi,bunge pia baraza
la sheria na katiba na kutoa ushauri pale inapobidi,
(d)
Anaweza
kufanya vikao na viongozi wa bunge,serikali ya wanafunzi,baraza la sheria na
katiba au wanafunzi kadiri aonavyo,
(e)
Kwa
kushirikiana na katibu wa wanafunzi na Raisi wa serikali ya wanafunzi, anaweza
kuandaa na kushirikishwa kama mjumbe katika kikao cha baraza la mawaziri na
kujadili ajenda au kutoa maamuzi na mazimio mbalimbali.
(f)
Anaweza
kutoa adhabu kwa mwanafunzi aliyeonesha utovu wa nidhamu kwa kushirikiana na
viongozi wa ngazi ya chini ya baraza la sheria na katiba.
(g)
Anapaswa
kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wote wanaishi katika mazingira safi na salama
kiulinzi na kiafya.
(5)Bila kuathiri mamlaka ya katiba hii yaliyopo kwenye ibara
hii,kutakuwepo na mlezi wa wanafunzi mwingine atakayejulikana kwa cheo cha
mlezi wa maswala ya kijinsia.
(a)
Kama
mlezi wa wanafunzi ni jinsia ya kike basi mlezi huyu atakuwa ni wakiume na kama
mlezi wa wanafunzi ni jinsia ya kiume basi mlezi huyu atakuwa ni wakike.
(b)
Mlezi
huyu atachaguliwa na utawala mkuu wa chuo.
(c)
Mlezi
huyu atapokea na kushauri maswala ya kijinsia ambayo mtoaji au mlalamikaji
anaona sio busara kuyapeleka kwa mlezi wa waanafuzi ambaye ni wa jinsia tofauti
kulingana na maudhui ya maswala husika.
(d)
Mlezi
wa jinsia hataruhusiwa kutoa maamuzi yatakayo sababisha kutolewa kwa adhabu
bila kupata kibali kutoka kwa mlezi wa wanafunzi ila maamuzi ya upatanishaji au
ushauri yapo chini yake.
SEHEMU YA PILI
12.ELIMU.
(1).Mwalimu
ambaye hatakidhi mahitaji ya somo; wanafunzi husika watapaswa kufikisha
malalamiko yao kwa wizara ya elimu ambayo itakuwa na jukumu la kupeleka kwenye
idara ya taaluma ya utawala wa juu wa chuo.
(a) Idara hiyo itapaswa kuyajadili na kuyafanyia kazi ikiwemo
kumbadilisha mwalimu mlalamikiwa.
(2).Walimu
watakaojiriwa na utawala wa juu wa chuo wanapaswa kukidhi vigezo vya mamlaka
husika zinazosimamamia elimu hapa nchini Tanzania ikiwemo Baraza la Taifa la
Elimu na Ufundi (NACTE).
(3). Gharama
za majaribio, ripoti na mitihani ziainiswe kwenye fomu ya kujiunga na chuo.
(4).Wizara
ya elimu itapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yake yote ikiwemo;
(a)
Kuhakikisha
wanafunzi wanafundishwa masomo yote na kwa kiwango au ubora stahiki.
(b)
Kufanya
kazi kwa karibu na Wawakilishi wa dadarasa ili kuchukuwa kero,mapendekezo au
maoni ya kitaaluma na kuyafanyia kazi.
(c)
Kutengeneza
sera na mipango mbalimbali itakayolenga kuboresha kiwango cha taaluma chuoni.
(d)
Ndio
waratibu na wasimamizi wa midahalo au mijadala ya kitaaluma chuoni.
13.HABARI.
(1). Idara
zote za habari zitakuwa chini ya wizara ya habari. Kutakuwa na idara kuu tatu,Idara
hizo ni;
(a) Idara ya redio.
(b) Idara ya runinga (tv) na,
(c) Idara ya magazeti.
(2). Wizara
ya habari itapaswa kutoa matangazo yatakayolenga kuwapata viongozi wa idara
hizo kuu tatu kwa muda wa wiki moja.
(a)
Mara
baada ya zoezi hilo kukamilika wizara itawafanyia usahili wote waliomba nafasi
hizo na kuteua waliofuzu.
(3).
Viongozi wa idara hizo hawataruhusiwa kuvifungua, kuvitengeneza, kuvifanyia
marekebisho yeyote au kuvipeleka kwa fundi au kwa kiongozi yeyote au mwalimu
bila ridha ya mwalimu mwenye dhamana husika.
(4). Mwalimu
wa idara husika atapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wizara na viongozi wa
idara husika.
(5). Wizara
ya habari pia itapaswa kuhakikisha ya kwamba idara zote zilizopo chini yake inazipangia
majukumu na kutimiza.
SEHEMU YA TATU.
14.NIDHAMU.
(1).Mwanafunzi
yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake,jukumu au kuonesha utovu wa
nidhamu, atapaswa kupewa adhabu.
(2).Adhabu
hizo zitatolewa na mwalimu wa chuo hiki au, Baraza la sheria na katiba.
(3).Kiongozi
yeyote wa serikali ya wanafunzi Hatokuwa na mamlaka ya kutoa adhabu baada ya
kupata kibali cha kufanya hivyo kutoka kwa baraza la katiba na sheria kwa ngazi
ya juu au wizara ya nidhamu au sheria na katiba.
(4). Adhabu
yoyote itakayotolewa isiwe ya kudhalilisha utu wa mwanafunzi,heshima
yake,jinsia au kwenda kinyume na haki za kibinadamu, ikiwemo kuchapwa fimbo,
kupigwa makofi au ngumi au kubeba vitu vizito.
(a) Msingi wa utoaji
wa adhabu utapaswa kuzingatia adhabu zile zenye
kulenga kumjenga mwanafunzi kitaaluma ikiwemo kufanya mazoezi ya
kimasomo zaidi.
(5). Bila kuathiri
masharti yoyote ya katiba hii adhabu itakayotolewa ni lazima iendane na uzito
wa kosa kama ilivyoainishwa kwenye, kanuni,sheria au katiba zote mbili yaani
katiba ya utawala wa juu wa chuo au katiba hii ya wanafunzi wachuo cha Uandishi
wa Habari na Utangazaji Arusha.
(4). Ni kosa mtu ambaye hana hatia kupewa adhabu
au kuchukuliwa kama mwalifu .
(a)Haitaruhusiwa kutolewa adhabu kwa kikundi cha watu kwa
kosa lilofanywa na mtu mmoja.
(5). Adhabu
itatolewa kwa mwanafunzi atakeyebainika kutoa mimba, kumuwezesha kwa kukusudia
aidha kiushauri au kifedha mwanafunzi mwingine kutoa mimba; adhabu hiyo yaweza
kuwa;
(a)
Kusimamishwa
masomo ,
(b)
Kufukuzwa
chuo,
(6).Bila kuadhiri masharti yoyote ya ibara hii
yaliyopo kwenye ibara ndogo ya (8), mtuhumiwa hata adhibiwa au kuchukuliwa kama
mhalifu hadi uthibitisho wa kitabibu kutoka kwa dakitari wa hosipitali inayotambulika
kisheria kuhusu tuhuma hiyo uoneshe kosa hilo na udhibitisho huo uwe na sahihi ya mganga mkuu
wa hosipitali hiyo.
(a)
Pili,
uthibitisho huo uoneshe dhamira ya mauwaji au ubainishe ya kwamba hakufanya
hivyo kutokana na sababu halali za kitabibu zinazotambulika na wizara ya afya
ya serikali ya Tanzania.
(7).Mwanafunzi
atakayechelewa kuingia darasani kabla ya
robo saa baada ya kipindi kuanza ataruhusiwa kuingia darasani, ila
atakaechelewa baada ya robo saa kipindi kuanza hatoruhusiwa kuingia darasani labda
kwa sababu maalumu au kibali cha mwalimu wa somo husika.
(a) Pia
mwanafunzi huyo hatoruhusiwa kuudhuria vipindi vinavyofuata mara baada ya
kipindi husika kumalizika.
15.SHERIA, KATIBA NA
UTAWALA BORA.
(1).Katika
hali yoyote serikali ya wanafunzi haitavunjwa, bali utaratibu ufuatao utakutumika
kama viongozi wake watakiuka misingi ya uongozi hali itakayopelekea kukosa imani kwa wanafunzi pia walimu.
(a) Mlalamikaji/walalamikaji wawe ni wanafunzi au walimu ambapo
watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa spika wa bunge au mbunge yeyote ili
afikishe kwenye kikao cha bunge.
(b) Mara baada ya bunge kupokea taarifa hiyo litafuata
utaratibu wa kumuondoa kiongozi huyo kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni zao na
katika hii au sheria nyinginezo.
(2).Adhabu
kutoka kwenye utawala wa juu wa chuo zitaruhusiwa mara baada ya uongozi wa ngazi
ya juu wa serikali ya wanafunzi kushirikiswa na kama uongozi huo utabaini utata
au udhaifu kwenye adhabu hiyo unaweza kutoa ushauri kwa utawala huo au kupeleka
kwenye baraza la sheria na katiba kwa ajili ya ufafanuzi wa kisheria ; adhabu
hizo zaweza kuwa: Kufukuzwa chuo kwa mwanafunzi,
(a)
Kusimamishwa
masomo au
(b)
Au
adhabu itakayopaswa kufanyika kwa zaidi ya muda wa wiki mbili.
(3).Utaratibu
wa bunge kutunga sheria,
(a)
Mbunge,spika
wa bunge au katibu wa serikali ya wananfunzi anaweza kupeleka bungeni
mapendekezo ya mabadiliko ya sheria au undwaji wa sheria mpya.
(b)
Mara
baada ya hatua hiyo bunge litapaswa kuikubali hoja hiyo kwa wingi wa idadi ya kura
za wabunge.
(c)
Baada
ya hoja hiyo kukubaliwa bunge litajadili mapendekezo hayo.
(d)
Bunge
litakaa kama kamati na kupitisha kifungu kimoja baada ya kingine cha
mapendekezo hayo.
(e)
Mapendezo
hayo yakishaapitishwa yataitwa mswada ambao utasubiri sahihi ya Rais ,Rais atalazimika
kuchukua maamuzi kwa siku zisizo zidi kumi na nne mara baada ya kupitishwa na
bunge.
(f)
Rais akisaini mswaada huwo utakuwa sheria na
kuanza kutumika rasimi mara baada ya kutangazwa kwa wanafunzi wote.
(4)Kama Rais
hatatia sahihi, bunge litalizimika kufanya yafuatayo;
(a)
Kujadili
mapendekezo au udhaifu ulioainishwa na Rais na kisha kuupitisha upya,
(b)
Au
kuupuza na kutokuujadili tena yaani kuachana nao.
(5).
Utaratibu wa kubadilisha katiba,
(a)
Bunge
litapaswa kuridhia zoezi hili kwa idadi nyingi ya kura,
(b)
Mara
baada ya kipengele hicho spika wa bunge ataunda kamati ndogo itakayokuwa na
wabunge wa tano, wawakilishi watatu wa madarasa pia Rais na mwenyekiti mkuu wa
baraza la sheria na katiba watakuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati hii.Kazi
kubwa ya hii kamati ni kuunda tume ya katiba itakayokuwa na wajumbe wasiopungua
kumi wala kuzidi ishirini.
(c)
Tume
hiyo itapaswa kukusanya maoni kutoka kwa wanafunzi wa chuo hiki.
(d)
Kuyajadili
maoni na kutengeneza rasimu ya kwanza ya katiba.
(e)
Rasimu
hiyo ya kwanza itarejeshwa kwa wanafunzi ili ijadiliwe.
(f)
Baada
ya hapo tumeitajadili maoni hayo ya
marekebisho na kuunda rasimu ya pili.
(g)
Tume
itaunda bunge maalumu la katiba litakalokuwa na wajumbe wawili wawili kutoka
kila darasa na wajumbe wote watume ya katiba.Bunge hili litajadili rasimu yote
na kupendekeza mapendekezo yake.
(h)
Mara baada ya mapendekezo tume ya katiba
itakaa na kuyajadili mapendekezo hayo,kisha kuyapeleka tena kwenye bunge hili
maalumu la katiba.
(i)
Bunge
maalumu la katiba litapitia hayomarekebisho ya tume na kisha kujiridhisha kwa
kupiga kura,ili hatua hii ifanikiwe wajumbe zaidi ya theluthi mbili watapaswa
kuiridhia rasimu hiyo.
(j)
Baada
ya rasimu hiyo kupita itaitwa rasimu ya pili ambayo itapelekwa kwa wanafunzi
kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni ya ndio au laa.
(k)
Rasimu
ya pili ikipitishwa na wanafunzi itapelekwa kwa Raisi na mkurugenzi wa chuo cha
Uandishi wa Habari na Utangazji Arusha kwa ajili ya kupata saini zao.
(l)
Mara
baada ya sahihi zao Afisa Uhusiano wa wanafunzi au waziri wa habari atapaswa
kutangaza kwa wanafunzi na hapo ndipo itakapoanza kutumika rasimi.
(6)Kama
mchakato huu wa katiba utakwama katika hatua yoyote ile basi tume italazimika
kufanyia kazi sababu za msingi zilizoikwamisha, ila sabau hizo lazima ziwe na
nia na dhamira njema.Pia kama mchakato huwo utakwama kwenye hatua ya kura za
maoni ya wanafunzi basi tume inaweza kuanza upya mchakato huo.Ila kama hatua
moja itarudiwa kwa zaidi ya mara mbili, bunge la wanafunzi kwa kushirikiana na
Raisi laweza kuivunja tume na kuunda nyingine.
SURA YA TATU.
MICHEZO, BURUDANI,AFYA,
NA MAKAZI.
SURA YA KWANZA
16.MICHEZO NA BURUDANI.
(1).Ununuzi
wa vifaa vyote vya michezo au burudani pamoja na shughuli zote andamizi
ikiwemo,uzinduzi wa vifaa/zana hizo,au uifadhi utapaswa kufanyika chini ya
wizara husika.
(2).Wizara
husika ikishirikiana na mwalimu husika pamoja na kamati/idara husika itakuwa na dhamana ya kuandaa na kuratibu
michezo,matamasha,ligi,bonanza na mashindano mbalimbali aidha ya ndani au nje
ya michezo.
(3). Uteuzi
wa kamati/idara za michezo/burudani na viongozi wote wa timu za chuo utakuwa
chini ya wizara husika.
(4).Kamati/idara
zote za michezo/burudani zitawajibika
kwa wizara husika .
(5). Wizara inayohusika na Michezo/burudani wakishirikiana
na mwalimu husika kwenye wizara yao watapanga utaratibu wa kuwapata viongozi wa
kamati/idara zao na majukumu yake.
(6).Usajili
wa vilabu au timu binafisi na vikundi mbalimbali vya michezo au burudani
utakuwa chini ya wizara husika kwa utaratibu watakaouweka; mara baada ya
usajili taarifa zitapaswa kwenda kwa mwalimu wa michezo au burudani na pia kwa
mlezi wa wanafunzi.
(7). Mwalimu
wa michezo/burudani, mwalimu yeyote au kiongozi yeyote wa wanafunzi hawatakuwa
na jukumu la kumkataa kiongozi au mjumbe yeyote wa kamati/idara ya michezo au
muundo au uwepo wa idara/kamati husika, bali jukumu hilo lipo chini ya wizara
yenye dhamana husika.
(8).Kama
mwalimu au kiongozi yeyote hataridhishwa na uteuzi au muundo pia uwepo wa kamati/idara
hiyo basi atapaswa kufuata utaratibu kama ulivyo ainishwa kwenye 4(iii),(b),(bb)
ya katiba hii.
(9).Fedha
yoyote itakayopatikana kwenye mashindano,tamasha,bonanza,ligi au chanzo
chochote ikiwemo fedha kutoka utawala wa juu wa chuo au serikali ya
wanafunzi zitakuwa chini ya wizara
husika (wizara ya michezo au burudani) kwa kusaidiana na mweka hazina wa kamati
au idara husika.
(10).
Mwalimu wa michezo au burudani atapaswa kushirikiana na wizara ya michezo/burudani
kabla ya kuchukua maamuzi yeyote yale.
(11).Wizara
ya michezo/burudani itakuwa na jukumu la kuifadhi na kukarabati vifaa au zana
zote za michezo.
17.AFYA NA MAKAZI.
(1).Hairuhusiwi
kwa wanafunzi zaidi ya wanne kuishi chumba kimoja.
(2).Wanafunzi
wenye jinsia tofauti hawaruhusiwi kuishi wala kulala chumba kimoja.
(3).Kiongozi/viongozi
wa hosteli watachaguliwa na wanafunzi wakazi wa hosteli husika chini ya
usimamizi wa wizara husika.
(4).Viongozi
wa hosteli watawajibika kwa wanafunzi na wizara husika.
(5).Kila
mwisho wa mwezi kisima/visima vya maji safi na vyombo vya kuifadhia maji vitapaswa kufanyiwia usafi pamoja na kuwekwa
dawa.
(6).
Mwanafunzi anayeishi hosteli au mtu mwingine yeyote haruhusiwi
kulewa,kutumia au kuwa na harufu yoyote
ya pombe,sigara, bangi, au madawa yoyote ya kulevya katika mazingira au maisha
ya hosteli.
(7).Utawala
wa juu wa chuo unapaswa kuhakikisha ya kwamba miundombinu yote ya hosteli iko
salama na inakidhi mahitaji,miundombinu hiyo ya weza kuwa;
(a)
Milango,geti,madirisha,sakafu,vioo,
pia vitanda au
(b)
Huduma ya maji au umeme.
(8).Utawala
wa juu wa chuo utapaswa kuhakikisha ya kwamba maeneo ya chuo ni masafi pamoja
na miundombinu yake ikiwemo vyoo,ukumbi na madarasa,zoezi la ufanyaji wa Usafi
halitapaswa kufanywa na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha.
(a)
Bila
kuathiri masharti yeyote ya katiba hii ,kifungu hicho hapo juu hakihusiki kwa
mazingira ya hosteli ambako wanafunzi watalazimika kufanya Usafi wenyewe.
SURA YA NNE.
MAADILI YA
WANAFUNZI,VIONGOZI, WALIMU NA WAJIBU.
SEHEMU YA KWANZA
18. MAADILI YA WANAFUNZI
(1)Mwanafunzi
atapaswa kufanya ya fuatayo;
(a)
kuheshimu,
katiba hii na katiba ya utawala wa juu wa chuo,sheria na kanuni zote za chuo.
(b)
Kuwaheshimu
wanafunzi wenzake, walimu, na wafanyakazi wote wa chuo.
(c)
Kuvaa
mavazi yenye maadili ya chuo, na kitanzania awapo chuoni au popote pale kwa
ajili ya maswala ya kitaaluma au akikiwakilisha chuo,
(d)
Kuvaa
aina ya mavazi kwa mujibu wa taratibu za chuo kwa siku husika,yaani kama ni
siku ya mavazi ya chuo au kama ni mavazi yeyote.
(2)Mwanafunzi hatapaswa kufanya yafwatayo;
(a)
Kuiba
mali au kitu chochote cha mwanafunzi au chuo ama kwa yeyote,
(b)
Kudharau
mwanafunzi yeyote au mwalimu ama mfanyakazi wa chuo,
(c)
Kufanya
vitendo vya kiburi,
(d)
Kukidhalilisha
chuo ndani au nje ya chuo,
(e)
Kutenda
mambo maovu akiwa chuoni au amevaa mavazi yanayokitambulisha chuo au akiwa na
nembo yoyote ya chuo popote pale,
(f)
Kubugudhi
wanafunzi wenzake wakiwa katika hali ya utulivu wakati wakusoma au katika
mazingira ya hosteli,
(g)
Kusema
au kutetea uongo na uovu,masengenyo kwa yeyote au vitendo vya udhalilishaji au
udhalilishaji wa kijinsia na uchochezi.
(h)
Kuvaa
mavazi yasiyoendana na maadili ya taaluma ya habari na yenye kudhalilisha utu
na jinsia yake.
(aa) Kwa mwanafunzi yeyote hatoruhusiwa kuvaa mavazi yatakayokuwa
yameishia juu ya magoti na
(bb) Mavazi yenye kuonesha maumbile ya mwili yenye kupaswa
kusitiriwa,
(cc) Mwanafunzi yeyote hatoruhusiwa kuva vazi chini ya kiuno,
19.MAADILI YA WALIMU KWA WANAFUNZI.
(1)Mwalimu
yeyote wa chuo hiki atapaswa kuwaheshimu wanafunzi wa chuo hiki, na kuepuka
vitendo vifwatavyo;
(a)
Lugha
zisizo na maadili ikiwemo zenye dharau,kejeli na matusi,
(b)
Uzalilishaji,
au kumfanya mwanafunzi apoteze heshima yake mbele ya wengine
(c)
Kumpiga
mwanafunzi aidha kwa kutumia fimbo (kumchapa),makonzi,ngumi,makofi na kadhaalika,
(d)
Uchochezi.
(2)Mwalimu yeyote hataruhusiwa kuwa na
mahusiano ya kimapenzi,kujamiiana au uchumba na mwanafunzi wa chuo hiki,bila
ridhaa maalumu ambayo itahusisha swala la uchumba tu, utaratibu ufuatao ndio
utakao tumika;
(a)
Taarifa
za uchumba zifikishwe kwa mlezi wa wanafunzi na waziri wa maadili wa serikali
ya wanafunzi, pamoja na mkurugenzi wa chuo.
(b)
Mlezi
wa wanafunzi kwa kushirikiana na waziri wa maadili watapaswa kufikisha taarifa
kwa wazazi au mlezi/walezi /mfadhili au mdhamini wa mwanafunzi.Kama mwanafunzi
huyu hana wazazi au mlezi/walezi /mfadhili au mdhamini basi taarifa zapaswa
kwenda kwa ndugu zake.
(c)
Baada
ya hatua hiyo wanafunzi wote watatangaziwa uhusiano huo.
(3)Mwalimu
hataruhusiwa kuvaa mavazi yatakayo kwenda kinyume na maadili ya kitanzani awapo
katika eneo la chuo au popote atakapokuwa akitekeleza majukumu yake kwa
mwanafunzi.
(4) Mwalimu
hatoruhusiwa kutoza fedha za masomo ya ziada au kwaajili ya shuhuli yoyote ile
kutoka kwa mwanafunzi au mfadhili wake kinyume na uratibu uliopo kwenye fomu au
mkataba wa malipo,aidha yawe ni makubaiano ya hiyari na wanafunzi husika.
(5)Bila
kuathiri mashariti yoyote ya katiba hii,katiba ya utawala,sheria na kanuni
nyinginezo; mwalimu hataruhusiwa kufundisha au kutoa kazi kinyume na ratiba au
taratibu za chuo au kitaaluma bila kukubaliana na wanafunzi,masomo hayo
yatakuwa ni yahiyari.
(6)Kwa
mwalimu yeyote atakayekiuka mashariti yoyote yaliyopo kwenye katiba hii,sheria
au kanuni;malalamiko yanapaswa kupelekwa kwa mlezi wa wanafunzi.Mlezi wa
wanafunzi atapaswa kuyachukulia hatua au kupeleka kwa mnadhimu wa chuo (utwala
wa juu wa chuo) au kwenye idara au ngazi nyingine husika za utawala wa juu wa
chuo.
20.MAADILI KWA VIONGOZI WA WANAFUNZI.
(1) (mahali
popote katika katiba hii neno viongozi wa wanafunzi linamana ya kiongozi yeyote
ambaye ni mwanafunzi aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kuwaongoza
wanafunzi popote pale katika chuo hiki)
Madaraka
anayopewa kiongozi wa wanafunzi ni dhamana na atatumia madaraka hayo na
kutekeleza wajibu wake kwa:
(a)
kuzingatia
masharti ya Katiba hii,kanuni na sheria nyinginezo;
(b)
kuheshimu
wanafunzi,walimu na wafanyakazi wote wa chuo, viongozi wenzake na ofisi
anayoitumikia;
(c)
Pia kulinda mali zote za chuo na wanafunzi,
(d)
kukuza
imani na heshima ya ofisi kwa wanafunzi;
(2) Ni
wajibu kwa kiongozi kuwatumikia wanafunzi
dhamana ya uongozi na heshima kwa
kiongozi wa wanafunzi itazingatia mambo yafuatayo: ‐
(a) uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa au
uchaguzi uliyo huru na haki;
(b) uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi na
kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati undugu, ukabila, udini, upendeleo, rushwa au
vigezo vingine visivyo sahihi;
(c) utoaji wa huduma pasipo upendeleo na kwa kufuata maslahi
ya wanafunzi kwa kuonyesha-
(aa) uaminifu katika utekelezaji wa kazi za wanafunzi/chuo;
(bb) wajibu wa kutangaza maslahi binafsi ili kuepuka
mgongano wa maslahi;
(d) uwajibikaji kwa wanafunzi katika kufanya uamuzi na
vitendo; na nidhamu na kujituma katika
kutoa huduma kwa wanafunzi.
(3)Kanuni za
Uongozi kwa kiongozi wa wanafunzi, akiwa
ama katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine,
atahakikisha kwamba mwenendo wake:
(a) hauruhusu kutokea mgongano wa maslahi kati ya
maslahi binafsi na maslahi ya uongozi wa wanafunzi;
(b) hauhatarishi maslahi ya wanafunzi kwa
ajili ya maslahi
binafsi; au
(c) haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi,wanafunzi au
chuo.
(4) Baraza
la mawaziri litapaswa kutunga kanuni zaidi zitakazosimamia maadili ya viongozi
wa wanafunzi.
(5) Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa
wa wanafunzi, kushiriki kuongeza au kwa namna yoyote ile, kuboresha maslahi
yanayohusu wadhifa alionao, na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya
yataanza kutumika kwa Kiongozi atakayekuja baada ya yeye kuondoka au kumaliza
muda wa kukaa madarakani, kama sivyo mfumo ufuatao wapaswa kutumika;
(a)
Kama
ni bunge litapaswa kupata kibali kutoka kwa baraza la katiba na sheria,
(b)
Kama
ni baraza la katiba na sheria au serikali ya wanafunzi,kibali kitapatikana
kutoka kwa bunge.
(6) Kiongozi
wa wanafunzi hataruhusiwa kushika nyadhifa mbili au zaidi au kutumikia Mihimili
ya uongozi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja; yaani bunge la wanafunzi,baraza la
katiba na sheria au serikali ya wanafunzi.
(7)Matumizi
ya mali ya wanafunzi/chuo
(a)
Haitaruhusiwa
kwa Kiongozi yeyote wa wanafunzi kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote
ya wanafunzi/chuo, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali,bunge au baraza la
katiba na sheria au chuo, kwa madhumuni ya kumpatia yeye binafsi au mtu
mwingine yeyote manufaa ya kiuchumi.
(8)Miiko yauongozi kwa kiongozi wa wanafunzi.
(a)
Bila
ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa wanafunzi
atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa wanafunzi, ikiwemo Miiko ya
Uongozi, itakuwa kama ifuatavyo:
(9 Kiongozi
wa wanafunzi hatopaswa:
(a)
kuvunja
au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b)
kutoa
au kupokea rushwa;
(c)
kujilimbikizia
mali kinyume cha sheria;
(d)
kusema
uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;
(e)
kutoa
siri za Serikali kinyume cha sheria;
(f)
kutumia
wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu,
jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(g)
kufanya
vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi, kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.
(10) Kiongozi wa wanafunzi atapaswa:
(a)
kuheshimu
na kuendeleza dhana ya uwajibikaji wa pamoja, kwa viongozi wanaohusika; na
(b)
kuheshimu
na kuendeleza maadili ya viongozi wa
wanafunzi, ikijumuisha:
(aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika
katika jamii;
(bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za Wanafunzi/chuo;
na
(cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia Kanuni
za Maadili na Mienendo ya
Viongozi wa
wanafunzi, Kanuni za Kudumu za viongozi wa wanafunzi na miongozo mbalimbali ya
Serikali na bunge la wanafunzi kuhusu viongozi wa wanafunzi.
(11) Kiongozi yeyote wa wanafunzi ambaye
anatuhumiwa na kuthibitika kwa makosa ya:
(a) kimaadili;
(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; pia
(c) wizi au ubadhirifu
wa mali za wanafunzi/chuo
(d)Au ufuska
atasimamishwa
uongozi mpaka suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu wa sheria au taratibu nyingine
zinazowahusu viongozi wa wanafunzi.
(12)Mara
baada ya uchunguzi kukamilika ,kama atakutwa na hatia anaweza;
(a)
Kuvuliwa
madaraka,
(b)
Kushushwa
cheo,
(c)
Au
kuomba radhi,
Kila hatua
ya adhabu itachukuliwa kulingana na uzito wa kosa.
SEHEMU YA PILI
21.WAJIBU WA MWANAFUNZI.
(1)Kila
mwanafunzi wa chuo hiki anapaswa kuzingatia yafuatayo;
(a)
kuja
chuoni kwa wakati na kuondoka kwa wakati ,
(b)
Kuzingatia
ratiba zote za chuo,
(c)
Kufanya
majaribio na mitihani kwa usahihi na kwa wakati,
(d)
Kushiriki
shughuli mbalimbali za kimasomo
(e)
Kutoa
ushirikiano chanya katika jambo lolote lenye maendeleo aidha kwa chuo au
maendeleo binafsi, kwa walimu, wanafunzi wenzake, viongozi wa wanafunzi au
kiongozi yeyote wa chuo pia wageni,
(f)
Kuwa
watulivu wawapo darasani au sehemu yeyote ya mafunzo aidha ya nadharia ua vitendo,
(g)
Kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa mwalimu/mkufunzi
au mtu mwingine yeyote aliyepewa dhamana hii kwa muda huo punde awapo
katika mafunzo,
(h)
Kutii
na kuheshimu katiba hii,katiba ya utawala,sheria, kanuni au taratibu zote
halali za chuo au serikali ya wanafunzi.
(i)
Kuishi
na wanafunzi wenzake,walimu, viongozi wa wanafunzi,au kiongozi na mfanyakazi
yeyote wa chuo; Kwa amani, upendo na kwa kuheshimiana.
(2) Bila kuadhiri mashariti yoyote ya katiba
hii,mwanafunzi yeyote atakayekuwa na sababu ya msingi itakayomfanya asitekeleze
wajibu wake kwa ufanisi atapaswa kuomba ruhusa au kutoa taarifa kwa mamlaka
husika.
22.WAJIBU WA MWALIMU
KWA MWANAFUNZI.
(1) Mwalimu
yeyote wa chuo hiki hanabudi kutekeleza wajibu ufuatao;
(a)
Kufundisha
kwa wakati na kwa utimilifu,
(b)
Kutoa
mazoezi na mitihani kwa mujibu wa mtaala,
(c)
Kuhakikisha
wanafunzi wanaelewa anachokifundisha,
(d)
Kujenga
na kudumisha amani,umoja nidhamu na mshikamano kwa wanafunzi na walimu dhidi ya
wanafunzi,
(e)
Kuhakikisha
viongozi wa wanafunzi wanatekeleza wajibu wao kikamilifu,
(f)
Kutekeleza
wajibu wao kama walezi na washauri wakuu wa wanafunzi,
(g)
Kusimamia
shuhuli zote za kila siku za chuo
SURA YA TANO
ULEZI WA DARASA,UCHAGUZI
NA UDHIBITI WA MATUMIZA MABAYA YA FEDHA.
SEHEM YA KWANZA
23. MWALIMU WA DARASA
(i)Kutakuwa
na mwalimu wa darasa ambaye atakuwa ndyie mlezi mkuu wa darasa.
(ii)Mwalimu
huyu atateuliwa na utawala wa juu wa chuo kupitia uataratibu watakaouweka.
(iii)Kama
darasa halitaridhishwa na utendaji au uwepo wa mwalimu huyu kutokana na sababu
za msingi, watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa waziri wa elimu atakayekuwa na
jukumu la kuyafikisha kwa mlezi wa wanafunzi ambayeatayajadili na akiona yana
mashiko atayafikisha kwenye idara yenye dhamana husika ya utawala wa juu wa
chuo.
(iv)
Majukumu ya mwalimu wa darasa.
(a)
Kuhakiki
maudhurio ya darasa lake,
(b)
Kuhakikisha
darasa lake lina nidhamu,
(c)
Kutekeleza
wajibu wake kama mlezi na mshauri mkuu wa darasa husika,
(d)
Kusikili
za kero za wanadarasa, maoni maombi na mapendekezo na kuyafanyia kazi au
kuyafikisha sehemu husika,
(e)
Kuhakikisha
darasa husika linafundishwa kwa kiwango na ubora unaostahiki,
(f)
Kujua
udhaifu na ubora wakila mwanafunzi ili kujua jinsi ya kuwasidia na kuwafanya
watimize malengo yao yakitaaluma,
(g)
Utatuzi
wa migogoro au kutokuelewana baina ya wanadarasa wake au na pande nyingine uko
chini yake kama mlezi mkuu,
(h)
Anapaswa
kujenga au kudumisha amani,upendo mshikamano na na umoja baina ya wanadarasa na
wanafunzi wengine pia dhidi yao na walimu.
SEHEMU YA PILI
24.WAWAKILISHI WA DARASA.
(1)Kutakuwa
na viongozi wawili kwa kila darasa ,
viongozi hawa wanaweza kuwa wajinsia tofauti au moja kutokana na utashi wa
darasa.Watawajibika kwa darasa husika,mwalimu wa darasa,wizara ya elimu na kwa
kiongozi mkuu wa serikali ya wanafunzi.
(2)
Watachaguliwa na darasa kwa Utaratibu wa upigaji kura.
(3) Kwaa
darasa jipya litapaswa kufanya uchaguzi huu baada ya muda wa mwezi mmoja mara
baada ya kuwasili chuoni,ila kwa kipindi hicho cha kabla ya mwezi moja wanaweza
kumteua/kuwateua viongozi wa muda mfupi.)
(4) Majukumu
ya Mwakilishi wa darasa.
(a)
Kufanya
shughuli zote kama alivyoagizwa na mwalimu,darasa au viongozi wengine wa wanafunzi kwa niaba au kwa ajili ya
wanafunzi wa darasa lake.
(b)
Kuzikusanya
kazi za wanadarasa na kuzipeleka kwa mwalimu pia kuzirejesha.
(c)
Kupeleka
malalamiko,madukuduku,maombi au maoni ya wanadarasa kwenye mamlaka husika.
(d)
Kujenga
au kudumisha umoja na mshikamano kwa wanadarasa.
(e)
Kutatua
migogoro au kutokuelewana baina ya wanadarasa,au darasa lake dhidi ya darasa
jingine,mwanafunzi au dhidhi ya mwalimu.
(f)
Kuhakiki
maudhurio ya wanadarasa na kutoa taarifa kwa mwalimu wa darasa au mamlaka
nyingine husika.
(g)
Kuhakikisha
ratiba ya msomo inafuatwa ikiwezekana kumfuata mwalimu wa somo husika.
(5)Kikao chochote atakachohudhuria au taarifa
yoyote atakayopewa atapaswa kuitoa au kutoa maudhui yake kwa wanadarasa.
(6)Hatoruhusiwa
kuchukua maamuzi yoyote yale yenye maamuzi makubwa kwa wanadarsa bila
kuwashirikisha kwanza.
SEHEMU YA TATU
25.TUME HURU YA UCHAGUZI YA WANAFUNZI
WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA.
(1)Kutakuwa
na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na
Utangazaji Arusha amabayo kiongozi wake mkuu atakuwa ni mwenyekiti wa tume hiyo.
(2) Bunge litapaswa
kutunga sheria zitakazoonesha mfumo na muundo wa tume,majukumu ya viongozi na
idadi ya wajumbe watume.
(3)Baadhi ya
majukumu yake.
(a)
Kuandaa
chaguzi huru na za haki,
(b)
Kusimamia
kampeni za uchaguzi,
(c)
Kuhakiki
vigezo na sifa za wagombea au waliomba katika nafasi husika,
(4) Sifa na
vigezo vya wagombea wa nafasi ya Ubunge,Katibu wa wanafunzi,Makamu wa
Rais,Afisa uhusiano na Spika wa Bunge.
(a)
Awe
ni mwanafunzi wa chuo hiki,
(b)
Asiwe
na sifa ya kufanya kosa/makosa mkubwa yaliyomsababisha kutumikia adhabu kuanzia
ya miezi miwili.Adhabu hiyo pamoja na kosa husika linapaswa kuthibitishwa na
Baraza la sheria na katiba ngazi ya juu ya kwamba ni sahihi kama sivyo
kipengele hiki hakitatumika kama pingamizi,
(c)
Asiwe
na hatia ya kutoa mimba,wizi,ufuska pamoja na vitendo vya ulevi vilivyokithiri
au matumizi ya madawa ya kulevya.
(d)
Asiwe
mlarushwa wala mtoarushwa
(e)
Muda
wake wa masomo uliosalia uwe ni kuanzia miezi sita kwaanzia tarehe ya uchaguzi
kufanyika ,
(5) Sifa na
vigezo vya mgombea wa nafasi ya Urais.
(a)
Sifa
na vigezo vyote vilivyopo kwenye ibara 25(4) vitatumika kama vigezo na sifa
kwenye nafasi hii ya Urais.
(b)
Vigezo
na sifa za ziada;
(aa) Ngazi yake ya kitaaluma ianzie ngazi ya
tano (level five),
(bb)Awe na
uzoefu wa uongozi wa kuongoza watu zaidi ya mia moja, waweza kuwa ukiranja
pindi alipo kuwa sekondari au katika serikali yeyote ya wanafunzi pia yaweza
kuwa wadhifa katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
(6)Utaratibu
utakaotumika ili kuwapata viongozi wa nafasi ya Uraisi,Makamu wa Raisi,Katibu
na Afisa uhusiano wa wanafunzi katika uongozi wa serikali ya wanafunzi.
(a)
Tume
huru ya uchaguzi itapaswa kutangaza nafasi hizo na kutoa fomu kwa
wahusika.Zoezi la uchukuaji fomu litakuwa ni la kipindi cha siku kumi.
(b)
Tume
itazihakiki fomu hizo ili kujiridhisha kama wahusika wamekidhi vigezo na sifa
za nafasi hiyo.
(c)
Wagombea
waliopitishwa na tume wataanza kampeni za uchaguzi kwa kipindi cha wiki
moja.Tume ya uchaguzi itapaswa kuhakikisha ya kwamba kampeni hizi haziwagawi
wanafunzi wala wagombea kutokana na itikadi za,kikabila,kidini,vyama vya siasa
wala kumdhalilisha mtu yeyote.Pia mgombea ataruhusiwa kuwa na meneja wake wa
kampeni atakayekuwa na uwezo wa kumpigia kampeni na hata kumwakilisha mgombea.
(d)
Uchaguzi
utafanyika katika sehemu ambayo haitajenga mashaka wala hofu kwa wagombea au
wanafunzi.Katika uchaguzi huu kila mgombea atachagua wakala wake atakayesimamia
zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura.
(e)
Tume
itamtangaza mgombea aliyepata kura nyingi kuwa mshindi.
(8)Ukomo wa viongozi/wajumbe wa tume ya katiba utafika pale
kiongozi atakapo hitimu masomo yake,kujiuzulu au kuondolewa madarakani au tume kuvunjwa
na bunge.
SEHEMU YA NNE
26.MKAGUZI WA HESABU NA
MATUMIZI YA FEDHA ZA VIONGOZI WA WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa
na idara ya mkaguzi wa hesabu na matumizi ya fedha za wanafunzi itakayowajibika
kwa bunge la wanafunzi na viongozi wake kuteuliwa na bunge.
(2) Itakuwa
na viongozi wakuu watatu ambo ni.
(a)
Mkaguzi
Mkuu ,
(b)
Mkaguzi
msaidizi na
(c)
Katibu.
(3)Majukumu
ya idara hii.
(a)
Kukagua
na kuhakiki matumizi na mapato yote ya fedha kwa viongozi wote wa
Bunge,Serikali na Baraza la sheria na katiba, katika ngazi zote yaani
wizara,idara na kila ngazia au cheo.
(b)
Ndio
watunzaji wa fedha za serikali ya wanafunzi kwa niaba ya wizara ya fedha
,wanaweza kuziifadhi kwa mhasibu mkuu wa chuo au kwa Utaratibu wataouweka.
(c)
Kwa
shirikiana na wizara ya fedha, wanawajibu wa kufuailia ulipaji wa fedha za serikali
ya wanafunzi kwa kupitia tarifa za malipo kutoka kwenye mamlaka husika
(d)
Wanawajibu
wa kutoa fedha kwa utaratibu maalumu ama watakavyopata kibali kutoka kwa waziri
wa fedha.
(e)
Mara
baada ya ukaguzi watapaswa kuto taarifa yao kwa bunge na wanafunzi.