Na OSCAR SAMBA.
Salamu zangu nyingi kwako ewe uliyemtanzania ama Raia yeyote katika taifa lolote lile duniani,salamu hizi zinawapendelea zaidi kwa wale wanamapinduzi yakidemokrasia na wapenda Haki.
Ambao kwao ushabiki uliyo chanzo cha upofu kifkra hautajwi kwao.
Siku chache zilizopita nilitoa taadhari kwa uma wa watanzania hususani wale wanaotambua dhana ya
Demoktrasia ya Haki,katika makala yangu niliwataadharisha Chadema kuwa wanapaswa kuwa makini katika Umoja wao wa Ukawa kwani wao ndio wenye nguvu zaidi na wasijaribu kutumia mwanya huo kuwakandamiza wagombea ama wanachama wa vyama vingingine katika ummoja huo.
Ninasikitika kwani sauti yangu haikusikika masikioni mwao,katika makala ile niliwaambia wanachadema kuwa wasikubali kumtoa mgombea Urasi na mwenza wake nikiwa ninahitaji kuwa wau vyama vingine vifanye pia hivyo,ila mambo hayakuwa vile kama nilivyo shauri.
Hali hii inaweza kuwa imechangiwa na wenzano wa CUF kufanya hivyo kule zanzibar kama ndivyo,lakini kihalali ingeitajika kwa upande wa Zanzibar pia kuwe na mchnganyiko wa vyma viwili na huku hivyo.
Kinachoendelea sasa kisiasa kinatafsiriwa kuwa "CHADEMA imeimeza UKAWA"haingi akilini eti Duni awe na uwezo mkubwa kuliko Pro. Limpumba ama Mbatia au Chadema kiwe ndicho chama chenye wagombea wenye nguvu ama uwezo mkubwa kuliko vyama vyote vingi; vitatu yaani NCCR MAGEUZI ,CUF na NLD.
Huu ni ulafi wa madaraka, ndivyo ilivyo katika majimbo pia ukifwatilia mgawanyo wa majimbo ni wazi CHADEMA imevimeza vyama vingine, Sina dhamira ya kuigawa UKAWA ila dhamira yangu ni ya dhati katima kuujenga umoja huu ukizingatia ndio umoja wa kwanza katika historia ya nchi yetu wenye mafanikio makubwa hadi sasa.
Nikukumbushe kuwa katika makala hiyo nilieleze adhari zake ikiwemo kuwakwaza wakina Pro. Lipumba na vyama vingine, hili limeshajidhiirisha,hakika hali hii ikifumbiwa macho nguvu ya UMOJA huu itafifia na kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao hali itakayo ijengea nguvu CCM zaidi.
Tafadhali niruhusu nichukuwe wasaa huu kukumbusha kuwa swala la ulafi wa madaraka ndani ya CHADEMA halijaaza leo kwani miaka michache iliyopita walipoingia bungeni wakiongoza kwenye bunge la Jamhuri kwakuwa na wabunge wengi waliwatenga wenzao na kuunda kambi rasimi bungeni wenyewe.
Sababu walizozitoa zilikuwa dhaifu na hafifu lakini chakushangaza bila kurekebishwa kwa sababu hizo walikuja tena kuunga nawaliowatenga,kwkuw amisingi mikubwa ya Sisasa za dunia siku ya eo ni masila wenzao waliposikia UKAW wakakubaliana nao na hatimae kwa pamoja wakatengeneza mipango.
Binafsi nilipoyasikia hayo yakuwa na mgombea mmoja niliweka taadhari mapema kwani nilifahamu lengo na shabaha iliyonyuma ya pazia mapema ila nilihoji sana iweje wakubaliane mapema hivyo,lakin nilidhani ya kwamba huenda tayari wameshakubaliana kuhusu ama nammna watakavyo wapata wawakilishi katika nji ya usawa na haki isiyo na ujanja ujana.
Ninatumia neno ujanja ujanja kwani haniingi akilini eti kila jimbo limsimamishe mgombea wake kulingana na jinsi chama husika kinavyokubalika zaidi kwenye kata ama jimbo hilo, jambo hili ni gumu na halina haki kwani chama kama NLD ambacho hakina mbunge wala diwani kitapata jimbo gani ama kitapata majimbo na kata ngapi ?
Wakati huu sio wakati wakujitoa kama ilivyo dhamira ya baadhi ya viongozi wenye nguvu latika vyama ndani ya UKAWA ila nikukaa katika meza ya makubaliano wazungu wanaita "Round Table" wakati mnaunda ukawa mlikaa kwa pamoja kwenye meza duara na sasa fanyeni hivyo.
CHADEMA nyie ndio wenye dhamna kubwa katika utanzu wa mgogoro huu jitaidini ili kuunusuru umoja huu unaonekana kuwa na nguvu katika Demokrasia na wale mashabiki wa UKAWA na CHADEMA wasiopenda ukweli ama uwazi nawataka wajifunze kupima hoja na uwazi hata kama unawauma.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago