Mwalimu mkuu wa shule ya Nigeria ambako wasichana zaidi ya 100 walitekwa nyara Jumatatu, ameomba wakuu wa Nigeria wafanye jitihada zaidi kuwakomboa wasichana hao.
Piya aliomba kundi linalowazuwia wasichana hao kuonesha huruma.Inafikiriwa kundi lilohusika ni la Waislamu la Boko Haram.
Afisa mkuu wa elimu wa jimbo la Borno amesema wasichana 44 wameweza kuwatoroka waliowateka nyara, na 85 bado wametoweka.
Lakini wazee wanasema wasichana wengi zaidi bado wametoweka.
Askari wa usalama, makundi ya wanamgambo na jamaa wanaendelea kuwasaka wasichana hao.