Miili zaidi imeendelea kuokolewa katika Pwani ya Korea Kusini baada ya meli kuzama jumatano
REUTERS/Kim Kyung-Hoon
Na Martha Saranga Amini
Maafisa usalama wanaochunguza ajali ya meli ya korea kusini wanamshikilia nahodha wa meli hiyo wakimtuhumu kuikimbia meli hiyo iliyozama siku kadhaa zilizopita ikiwa na watu mia nne sabini na sita wakati huu waokoaji wakipata miili zaidi ndani ya meli hiyo.
Lee Joon-Seok na manahodha wenzake wanashikiliwa katika kituo cha polisi mapema asubuhi wakisthakiwa kwa kuiacha meli na kushindwa kuokoa maisha ya abiria kwa mujibu wa sheria za usafiri wa baharini.
Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 69 amekosolewa kwa kuitelekeza meli ilipokuwa ikizama jumatano asubuhi katika pwani ya kusini magharibi ikiwa n mamia ya abiria waliokwama ndani ya meli wengi wao watoto wa shule.
Takribani watu 29 wamethibitika kupoteza maisha kufuatia janga hilo huku watu 273 bado hawajulikani walipo.