Raia zaidi wa Burundi wameendelea kuukimbia mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura kutokana na kuendelea kuzorota hali ya usalama katika mji huo.
Watu wanne waliuawa katika mitaa miwili ya Bujumbura siku ya Jumatano. Mauaji ya mara kwa mara katika mji mkuu Burundi yamezusha wasiwasi mkubwa na kuwafanya baadhi ya raia wa mji huo kukimbilia katika nchi jirani za Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Asasi mbalimbali za kieneo na kimataifa zimeendelea kutahadharisha kuhusiana na mauaji yanayofanywa nchini Burundi. Hivi karibuni Nkosazana Dlamini-Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika aliripotiwa akisema kuwa, kuendelea machafuko nchini Burundi, kunaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika hali mbaya ya machafuko.
Burundi ilitumbukia katika hali ya mchafukoge tangu mwezi Aprili mwaka huu, baada ya chama tawala cha CNDD-FDD, kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu, hatua ambayo ilitajwa na wapinzani kuwa ni kinyume cha katiba na makubalino ya mjini Arusha, Tanzania.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago