Aliyefariki ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.
Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba
za Askari Polisi zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za
Polisi kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga
barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe
magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka
kituo cha Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku
Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa
kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya watu.