Wachezaji wa Simba wakisalimiana na wachezaji wa Coastal Union kabla ya mchezo kuanza.
Na Burhani Yakub na Sosthenes Nyoni, Mwananchi (email the author)
Posted Ijumaa,Agosti9 2013 saa 11:48 AM
Kwa ufupi
Kato alifunga mabao yote mawili katika mechi ya kwanza ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, kisha akafunga pia mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Yanga iliyokwisha kwa sare ya bao 2-2.
Coastal Union imefanya usajili wa nyota wengi msimu huu.
Tanga. Kiboko ya Simba na Yanga, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Yayo Kato, amesema mapokezi makubwa aliyopata kwa timu yake mpya, Coastal Union ya Tanga, atayalipa kwa kufunga mabao mengi msimu huu.
Wagosi hao wa Kaya, wamemsajili nyota huyo kutoka klabu ya URA ya Uganda, wakizipiku Simba na Yanga ambazo nazo zilikuwa kwenye mpango wa kumsajili.
Vigogo hivyo vilipata hamu ya kumsajili Kato baada ya kuvutiwa na kiwango chake wakati timu yake URA ilipokuja kucheza mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu hizo za Dar es Salaam.
Kato alifunga mabao yote mawili katika mechi ya kwanza ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, kisha akafunga pia mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Yanga iliyokwisha kwa sare ya bao 2-2.
“Katika maisha yangu sikuwahi kuota kama kuna siku nitakuja kupokewa kama mfalme. Naona hili ni deni kubwa kwangu mbele ya mashabiki wa Coastal Union,” alisema Kato.
“Kama kuna malipo kwa hiki nilichokiona hapa Tanga, basi ni kuhakikisha nalipa mapokezi haya mazuri kwa kufunga mabao mengi msimu huu.
“Nitahakikisha Union inakuwa juu ya Simba na Yanga. Nitajitahidi kufunga mabao mengi msimu wangu
www.hakileo.blogspot.comwa kwanza ili kuiwezesha Union kutwaa ubingwa,” alisema.
Yayo aliweka saini ya kuchezea klabu ya Coastal Union Jumanne wiki hii kwenye Hoteli ya Africana, Kampala Uganda ambapo atacheza kwa miaka miwili.
Kuhusu kutaka kusajiliwa na Yanga, Yayo alisema taarifa hizo hazina ukweli. “Nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa nimesajiliwa na Yanga, taarifa hizi hazina ukweli,” alisema.
“Kuna magazeti kama New Vision yamesema mimi nimesaini Yanga ukweli ni kwamba walikuwa wakiniwania kwa nguvu zote, lakini mapenzi yangu yapo Coastal Union kwa sababu niliipenda tangu tulipocheza nayo mchezo wa kirafiki.“
Msemaji wa Union, Edo Kumwembe alisema klabu yake imemsainisha mkataba wa miaka miwili baada ya kuridhika na afya yake kufuatia vipimo alivyofanyiwa.