Halmashauri zashauriwa kuunda chombo kusimamia maendeleo

Na Martha Fataely, Mwanga

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw. David Msuya, amezishauri Halmashauri za Wilaya, mkoani Kilimanjaro, kuunda chombo ambacho kitasimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi.

Bw. Msuya alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga pamoja na kuweka mikakati ya kusukuma maendeleo wilayani humo.

Alisema kazi kubwa ya chombo hicho ni kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo na kutafuta njia ya kupata fedha za utekelezaji ili kuhrakisha maendeleo ya wnanchi.

Bw. Msuya ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo mkoani Kilimanjaro (KDF), alisema vyombo hivyo vitafanya kazi karibu na mfuko huo ili kuhakikisha miradi husika inatekelezwa.

“Fedha za miradi zimekuwa zikitumwa, kuna watu ambao wanapaswa kutekeleza miradi hii lakini tunahitaji watu wengine ambao watakuwa wanaifuatilia kwa karibu ili isikwame,” alisema.

Awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Athuman Mdoe, wamepata mwekezaji kutoka nchini India ambaye anataka kujenga kiwanda cha kutengeneza juisi na tayari ekari 3,000 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha miwa ya kiwanda hicho.

Alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa eneo la Kifaru na kitasaidia kuongeza mapato ya halmashauri, wnanchi na kutoa ajira kwa vijna mkoani humo
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company