Obama aunga mkono diplomasia Syria lakini shambulizi la kijeshi bado lawezekana

HABARI ZETU
wwww.hakileo.blogspot.com
Obama akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni kuhusu maamuzi yake huko Syria.

Rais Obama ameeleza mpango wake wa kuzuia serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali jumanne na rais aliunga mkono kwa tahadhari pendekezo la Russia kutanzua mzozo huo.

Obama amesema shambulizi la Marekani huko Syria litakuwa lenye malengo maalum katika kuharibu matumizi ya kemikali.

Rais amesema hatapeleka wanajeshi wa Marekani huko Syria na hatafanya operesheni isiyojulikana mwisho wake kama vile Iraq na Afghanistan na mashambulizi ya ndege ya muda mrefu kama ilivyokuwa Libya au Kossovo.

Amesema anajua hali mbaya ya vifo viliyosababishwa na vita vya Iraq na Afghanistan , kwamba wazo lolote la vita halitapendwa na watu
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company