Aua baba kugombea urithi

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamtafuta Charles Ndelemo kwa tuhuma ya kumuua baba yake mzazi kwa kumpiga risasi akiwa na wenzake wawili na kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwalwanda alimtaja marehemu kuwa ni Protazia Ndelemo, na kwamba tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Ntantumbila wilayani Nkasi ambako inadaiwa kuwa hapo awali kulikuwa na ugomvi wa kugombea mali kati ya mzazi huyo na watoto wa mke wake mkubwa.

Alisema kuwa mke wa kwanza ambaye ni mama yake mtuhumiwa, alikuwa ameachana na Ndelemo, hivyo watoto wa mke mkubwa walikuwa wakidai kupewa sehemu ya mali, kwa madai ya kwamba mali hizo walichuma na mama yao ambaye ameachwa.

Kwa mujibu wa kamanda, mali zilizokuwa zinadaiwa ni mifugo na mashamba, lakini hakuna mali wala fedha zilizochukuliwa kwani mtuhumiwa na wenzake walitoweka mara baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Alisema kuwa polisi walifika katika eneo la tukio usiku, lakini hawakuweza kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alitambuliwa na mke mdogo wa marehemu, Limi Kuyela.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi linaendelea na msako wa kuwakamata watuhumiwa ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company