Wakati sherehe ya kuadhimisha siku ya Mashujaa inakaribia, serikali ya Kenya imeongeza nguvu katika kuimarisha hatua za kulinda usalama huko Nairobi. Kamishna wa mkoa wa Nairobi Njoroge Ndirangu amewaambia waandishi wa habari kuwa, idadi ya walinzi wa usalama itaongezwa mjini humo ili kukabiliana na tishio lolote la kigaidi.
Bw. Ndirangu pia ametoa ahadi kwa wakenya kuwa, serikali ya nchi hiyo imechukua hatua halisi ili kuhakikisha usalama wao jumapili wakati sherehe hiyo itakapofanyika.