Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto leo amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), licha ya viongozi wa Afrika kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta nchi hiyo iakhirishwe.
Ruto amewaambia waandishi habari akiwa huko The Hugue kwamba, anaona ni bora kesi yake iendelee lakini aruhusiwe kutohudhuria vikao vya kesi hiyo ili aweze kutekeleza majukumu yake nchini Kenya. Kenyata na Ruto wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Mwishoni mwa wiki viongozi wa Afrika katika mkutano wao uliofanyika huko Addis Ababa walikosoa vikali utendaji wa mahakama ya ICC wakilalamika kuwa korti hiyo inabagua na kuwafuatilia tu viongozi wa Afrika. Pia walilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuakhirisha kesi ya Rais wa Kenya kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa kifungu nambari 16 cha Mkataba wa Roma.