SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI LAENDESHA KAMPENI YA CHAKULA NA LISHE BORA TANZANIA



Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika na utapiamlo 42% ya watoto chini miaka 5 wamedumaa Asilimia 16 ya watoto wana uzito pungufu nchini

Na Moblog Team — Shirika la Chakula Duniani (WFP) Tanzania, Kwa kushirikiana Na Shirika la Chakula Na Kituo cha Lishe Tanzania (TFNC) na MuDA Africa, wafanya kampeni maalum ya elimu iliyoambata na ngoma katika kuelimisha umma umuhimu wa chakula bora kwa ajili ya afya ya jamii jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika soko la mabibo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mahusiano wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Fizza Moloo amesema kwamba shirika hilo limeamua kuendesha kampeni hiyo iliyoambatana na ngoma za asili ili kuelimisha jamii umuhimu wa chakula bora na lishe sahihi kwa ajili ya kulinda afya ya watumiaji.

"Tumemua kuwa na kampeni hii ya elimu juu ya chakula bora kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ili kupitia hadhara hii basi

elimu hii ya chakula na lishe bora iweze kufika maeneo yote nchi nzima mpaka mikoani,' amesema Moloo.

Moloo amesema kwamba wameamua kutumia njia ya ngoma kwa vijana kucheza katika kurahisisha kupeleka ujumbe huu mahusus kwa jamii ili wananchi waweze kupata elimu sahihi juu ya lishe bora kwa afya ya mtu moja moja na jamii kwa ujumla.

Amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika sana na utapiamlo katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara ikiwa na asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 wamedumaa na asilimia 16 wana uzito pungufu.

Moloo alifafanua kwamba watoto sita kati ya kumi wenye umri kati ya miezi 6-59 wana upungufu wa wekundu wa damu (DHS, 2010), amesema lishe duni ni tatizo kubwa kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa, wakati zaidi ya nusu ya wanawake wajawazito wana upungufu wa damu.

Amesema Mpango wa Chakula duniani umedhamiria kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia malengo yanayohusiana na lishe kwa mujibu wa Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA 11) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Lishe (2011-2016).

Kwa upande wao, mmoja wa wafanyabiashara wa soko la mabibo, Ratifa Mbwambo amesema wanalishukuru shirika la Chakula duniani kwa kuhamasisha jamii umuhimu wa kuwa na chakula na lishe bora kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

"Kwa kweli tunawashukuru sana kwa kuja katika soko letu la mabibo na kuelimisha watu umuhimu wa chakula bora kwa njia ya kupangilia mlo sahihi kwa kila siku," amesema.

Amesema ni muhimu kwa shirika hilo kufanya kampeni za namna hii mara kwa mara katika kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa kulinda afya ya jamii nzima kwa ujumla na vile vile elimu iendelee kutolewa ili watu wajifunze kadri iwezekanavyo.

Source: http://www.wavuti.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company