Ufichuaji wa taarifa za kudukuliwa kwa mawasailiano ya simu ya mkononi ya Merkel na idara ya usalama wa taifa ya Marekani NSA, umesababisha hasira nchini Ujerumani, na kuilaazimu serikali kumuita balozi wa Marekani kutoa maelezo. Der Spiegel lilisema idara maalumu ya kukusanya taarifa ilikuwa ikitumia vifaa vya kisasa zaidi kuichunguza serikali ya Ujerumani kutokea ubalozi wa Marekani mjini Berlin.
Kwa kutumia waraka wa siri wa mwaka 2010, jarida hilo liliongeza kuwa NSA ilikuwa inaendesha vituo vingine 80 sawa vya ujasusi duniani kote. Serikali imesema kuwa maafisa wa idara ya ujasusi ya Ujerumani watasafiri kwenda mjini Washington kukutana na wenzao katika wiki zijazo ili kupata maelezo.