Libya yaombwa kukabidhi Saif al-Islam kwa ICC

Saif al-Islam,mwanawe kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi, Julai 30, 2007.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa –ICC ametoa mwito kwa Libya kumsalimisha Saif al-Islam Ghadafi, mwanae kiongozi wa zamani wa Libya aliyeuawa Moammar Ghadafi, lakini mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa amesema ombi hilo limekataliwa.

Mwendesha mashtaka huyo wa ICC, Fatou Bensouda anataka utawala wa Libya uikabidhi mahakama hiyo mwana wa kiume wa Ghadafi Saif al- Islam kwa makosa mawili ya uhalifu dhdi ya binadamu; mauaji na mateso.

Bensouda alikuwa akizungumza na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamis mjini New York akisistiza kuwa ikiwa hati ya kukamatwa kwa mtuhumiwa imetolewa sharti iheshimiwe na kwamba maswala ya kisiasa hayana msingi katika sheria.

Lakini balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa Ibrahim Dabbashi aliliambia Baraza hilo la Usalama kwamba wananchi wa Libya wanataka kuona Saif al-Islam Ghadafi akishatkiwa nchini Libya.

Akizungumza kupitia mkalimani, balozi Dabbashi alisema hakuna serikali yoyote ile itakayokubali kesi hiyo kusikilizwa nje ya Libya kwa sababu itavuruga amani na uthabiti wa kijamii nchini Libya na kuleta hatari na vitisho zaidi kwa maisha ya wananchi.

ICC ilikubali kesi ya mtuhumiwa mwingine wa Libya ambaye zamani alikuwa mkuu wa idara ya kijasusi, Abdullah al-Senussi isikilizwe Libya na hivyo balozi Dabbashi anasema haoni kwani nini ICC isiiachie Libya kusikiliza kesi dhidi ya Saif.
www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company