Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Nigeria imesema rais Goodluck Jonathan ameugua akiwa London na ameshauriwa kupumzika kwa siku kadhaa.
Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema bwana Jonathan alitakiwa kuhudhuria mkutano wa uwekezaji katika mji mkuu wa Uingereza Alhamis lakini hakuweza kushiriki.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa hali ya rais Jonathan si mbaya sana lakini imebidi tahadhari ichukuliwe na anapewa matibabu.
Rais huyo wa Nigeria alifikisha umri wa miaka 56 wiki hii. Ameshika wadhifa wa urais wa Nigeria tangu mwaka 2010. Nchi hiyo ni maarufu kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika.
www.hakileo.blogspot.com
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago