Wanaharakati watowa wito kuimarisha vita dhidi ya ubakaji Afrika Mashariki


Kundi la watu wakiandamana kuiomba serikali ya Afrika Kusini kuchukua hatua kali dhidi ya ubakaji. Februari 27, 2013, mjini Cape Town.
Katika kipndi cha "Live Talk", Saida Ali mkurugenzi wa Shirika la kupambana na Dhulma dhidi ya Wanawake nchini Kenya, COVAW, anaema tatizo la ubakaji limeongezeka na kunahitajika juhudi za pamoja kuelimisha watu na kupambana na janga hilo.

Lilian Liundi mkuu wa kitengo cha habari cha mtandao wa jinsia TGNP nchini Tanzania anasema vitendo vya dhulma na ubakaji dhidi ya wanawake vinaongezeka siku hadi siku.

"Katika uchunguzi uliofanywa 2002 kulikuwepo na wanawake 3 331 waloripoti kubakwa na uchunguzi kama huo ulofanywa 2007, unaonesha kulikuwepo na wanawake na wasichana 8 774 waloripoti kubakwa. Hiyo ni ongezeko kubwa kabisa na hao ni wale wanaripoti kwani wengi wanaogopa kuripoti kuwa wametendewa vitendo vya dhulma." anasema Bi.Liundi.

Nae Mkurugenzi wa kundi linalowasaidia walonusurika na ubakaji Kenya GVRC Bi. Alberta Wambua, wengi wa wanawake na wasichana wahaoomba msaada kutoka kundi lake, wanakuwa waoga kwenda kuripoti juu ya vitendo viovu waloshuhudia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company