Mohammad Javad Zarif
NA RADIO TEHRAN
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema, 'Jamhuri ya Kiislamu itasimama kidete mbele ya kiongozi yeyote wa kigeni ambaye atathubutu kuvunjia heshima wananchi na Mapinduzi ya Kiislamu.'
Zarif ameyasema hayo leo Jumatano katika kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran. Ameashiria matamshi dhidi ya Iran ya Barack Obama Rais wa Marekani katika hotuba aliyotoa katika kituo cha Kizayuni cha Saban na kuongeza kuwa, 'Rais wa Marekani amefikia natija kuwa hawezi kusimamisha urutubishaji madini ya urani nchini Iran.' Zarif ameendelea kusema kuwa matamshi ya Obama kuwa iwapo Washington ingekuwa na uwezo ingefunga kabisa miradi ya nyuklia ya Iran ni kukiri wazi kushindwa Marekani mbele ya Iran. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameendelea kusema kuwa hakuna shaka kuwa Iran inaweza kuanza tena urutubishaji madini ya urani kwa asilimia 20 katika kipindi cha masaa 24. Amesema Iran inabainisha misimamo yake imara kwa lugha ya kidiplomasia. Zarif ameashiria namna wakuu wa utawala wa Kizayuni walivyoingiwa na hofu kufuatia Mapatano ya Nyuklia ya Novemba 24 kati ya Iran na kundi la 5+1. Ameongeza kuwa: 'Mazungumzo ya Geneva yamesambaratisha mazingira batili ya hofu dhidi ya Iran yaliyokuwa yametengenezwa na Wazayuni. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema wanaofanya mazungumzo kwa niaba ya Jamhuri ya Kiislamu wanajitahidi kuhakikisha kuwa heshima na misingi ya mapinduzi inalindwa.