Salva Kiir yuko tayari kwa mazungumzo.

Wananchi wanaotafuta hifadhi wakielekea makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Juba Dec. 18, 2013.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na mpinzani wake makamu rais wa zamani anayemtuhumu kuongoza jaribio la mapinduzi dhidi yake.

Umoja wa mataifa unakadiria siku 4 za mapigano huko Sudan Kusini yameuwa watu wapatao 500.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa amemsihi rais Salva Kiir kufanya mazungumzo na wapinzani wake na kushirikiana na Umoja wa mataifa wakati huu wa msuko suko nchini mwake.

Bw.Ban amesema watu wapatao 20,000 wameomba hifadhi kwenye ofisi za Umoja wa mataifa kwenye makao makuu huko Juba . Maafisa wa Sudan Kusini wamewataka wakazi kurudi majumbani mwao kufuatia mapigano hayo makali.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company