20 WAFARIKI KWENYE MLIPUKO DRC


Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghala la silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo ,vimesema kuwa nyumba nyingi zilaharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi. (JM)
Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radi

Kwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco,zaidi ya watu 50 pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.

Lengo la Monusco nchini humo ni kupokonya makundi yanayopigana silaha. DRC inajaribu kutokamana na vita vilivyosababisha mamilioni ya vifo kati ya mwaka 1998 na 2003.

'Nimewaamrisha maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi hicho cha Monusco.

Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi. CHANZO BBC SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company