YANGU NDANI
YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAEENDELEO (CHADEMA)
Nilijiunga
na chama cha democrasia na maendeleo{CHADEMA} mwaka 2005 nikiwa na umri wa
miaka 15
nikiwa
naingia kidato cha Kwanza kwa mujibu wa katiba ya chadema Sura ya Tano 5.1.7
vijana wenye umri wa miaka 12-17 wanajiunga na chama kama wafuasi wa chama na
kupewa kadi maalumu ya baraza la vijana chadema name nilifanya hivyo.Sikujiunga
na chadema kwa
ushawishi wa
mtu yeyote ila mwaka 2005 Mbowe alipo simama kama mgombea uraisi niliamua
kujiunga na chadema kutokana na sera
nzuri itikadi nzuri,falsafa na ilani
yenye matumaini kwa mtanzania hasa msaka tonge.
Sijawahi
kuwa na hofu hata kidogo juu ya chama changu nikiamini siku moja kilio cha
watanzania kitakuja kuisha nimekua na kupata elimu yangu huku nikitangaza sera
nzuri ya chadema na kushawishi watu wengi kuingia kunako ukombozi wa kweli, japo
ilikua nijukumu langu kwa mujibu wa katiba Sura ya tano 5.3.3
Naandika
waraka huu nikiwa mwanachama halali wa chadema na wakawaida sana ambapo
nikiongozi
wa ngazi ya
chini kabisa ya muundo wa chama nikiwa katika ngazi ya misingi inayotambulika
kikatiba 6.1.1 Kwakua chama changu kina amini juu ya democrasia ya kweli pomoja
na uhuru wakutoa maoni.Makamanda tunaamini Chadema ni mpango wa Mungu CHADEMA
kimekua chama
pendwa na
watanzania tukiamini ndio tumaini letu na kimbilio la masikini,wanyonge,na
wapenga
maendeleo
nadhubutu kusema ni hama chenye watu
wenye upeo mkubwa tukiwa tunaamini 2015
tunaenda
kuishika dola…..
MAONI YANGU
JUU YA MGOGORO NGANI YA CHAMA Kwanza nadhubutu kusema kutokama na mgogoro ulio
tokea umeishusha chadema katika mbio zake zakujiandaa kuishika dola zaidi ya asilimia
45 kwani wengi kwa sasa wapo katikati na hata ndani ya wanachama wa chama
kimoja huzozana na kugombana nakujipa makundi
eti kujiita TEAM ZITO na
TEAM CHADEMA
Mgogoro ndani ya chama umewapa nafasi
kubwa wasiokitakia mema chadema kutumia fursa kukichafua chama{Nape tarehe
8/1/2014 T.B.C na wengineo Chadema
kimepoteza wafuasi wake kutokana na maneno ya kuchafuana kati ya ZITO na MBOWE
kwa kukosa
uaminifu kwa
viongozi wake SIASA ZA MITANDAONI KWA VIONGOZI Mitandao ya kijamii imekua
kikwazo kikubwa ndani ya vyama vya siasa
kuchafuana kwa uchunguzi nilio ufanya wanasiasa wengi wanaoshinda kwenye mitandao ya kijamii wamekua wakichukua nafasi kubwa kutupiana matusi na
kuchafuana ZITO NA LEMA ni mfano mzuri na kila kinachotokea badala ya
kukifikisha katika sehemu
husika
huwekea watu mitandaoni Nape aNauye alikua
na tabia hiyo nadhani kaonywa kwa hilo litazamwe kwa jicho la pekee…
PENDEKEZO
KUTOKANA NA MGOGORO
Sipo katika
upande wa zito hata kidogo ila BUSARA lazima itumike katika kutatua matatizo na
migogoro
ndani ya
chama kutumia jazba haito saidia hata kidogo bali nikukitakia chama Matatizo mnapaswa kutambua mamilion ya watu hutegemea chadema kama mkombozi wake naandika waraka
huu nikiwa natokwa na machozi kwani tangu chadema imeingia katika mgogoro
nimekua naumwa na kukosa raha na dhani kwa maneno haya kidogo ntahisi nimeutua mzigo Sijawahi kuwaza kuhama chadema ila
migogoro
ngani wa wanachama inaniumiza wakati
busara ikitumika tunaweza kukaa pamoja na kumaliza tatizo
HITIMISHO
Kamati kuu
kaeni chini nakuwaza matumaini ya Watanzania yapo ndani ya chadema na bado tunaliamini hilo tumieni
busara kuyaunganisha haya makundi
yaliyojitokeza ndani ya
chadema na
sisi wanachadema si vyema kuwa washabiki
wa mpasuko huu
MUNGU
IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI CHADEMA.