MJENGWA; SERIKALI TATU: TUMWAMINI NANI, JAJI AU MWANASIASA...?



Ndugu zangu,
Nimepata kusema, kuwa haiyumkini Majaji wetu hawa wazaliwa na wazalendo wa nchi hii wakawa wote wana matatizo katika kufikiri kwao; Jaji Francis Nyalali, Jaji Robert Kissanga, Jaji Joseph Warioba na Jaji Augustine Ramadhan . Na nikamsahau Jaji Mark Bomani. Kwamba wote hawa, na katika nyakati tofauti, wamependekeza mfumo wa Serikali Tatu ili kuunusuru na kuuimarisha Muungano wetu.

Nahofia, kuwa baadhi ya wanasiasa wetu ndio wenye matatizo katika kufikiri kwao. Kwamba wanaangalia kwanza ni mfumo gani wa Serikali utakaowanufaisha wao binafsi, makundi yao na vyama vyao kwa kuangalia namna watavyoshinda chaguzi za kisiasa na kushika madaraka.

Wanaangalia zaidi leo na kesho. Kwao kesho kutwa na mtondogoo ni mbali sana.

Naam, tumwamini nani? Maana, iliimbwa, kuwa ' Mwanasiasa' ni ' kigeugeu! Na Jaji naye....?
Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.
0754 678 252
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company