Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa nchini Marekani amesema kuwa mikono michafu ya Marekani na utawala wa Israel ni chanzo cha mizozo inayoendelea sasa huko Sudan Kusini na katika bara zima la Afrika. Akizungumza na televisheni ya Press yenye makao yake hapa Tehran, Stephen Lendman ameyataja machafuko makubwa ya Sudan Kusini kuwa ya kusikitisha na kusisitiza kwamba mikono michafu ya Washington na Tel Aviv ndio chanzo cha hali hiyo.
Lendman amesema pia kwamba serikali inayopenda vita ya Marekani na waitifaki wake ni sababu kuu iliyopelekea Sudan Kusini kujitenga na Sudan mwaka 2011. Machafuko yalizuka huko Sudan Kusini tarehe 5 mwezi Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kumtuhumu makamu wake za zamani Riek Machar kuwa amejaribu kuipindua serikali yake. Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa wa Marekani amesema utawala wa Tel Aviv na waitifaki wake wa Magharibi unahusika pakubwa katika migogoro mikubwa inayotokea katika nchi za Kiafrika.