Sheikh Mkoa wa Mara afariki dunia

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Mara, Othman Magee, amefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na saratani ya kibofu.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) limekipokea za kifo hicho kwa masikitiko makubwa. “Baraza linatuma salamu za pole kwa Waislamu wote wa mkoa huo kwa kuondokewa na kiongozi wao huyo wa kidini. Pia Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira wanafamilia wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao,”alisema Alhad.

Kwa mujibu wa mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu huyo, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema awali Sheikh Magee alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kabla ya kuzidiwa na kuhamishiwa Muhimbili hivi karibuni.

Mwili wa marehemu Sheikh Magee ulitarajiwa kusafirishwa jana kuelekea nyumbani kwake Mtaa wa Kennedy, Kata ya Mwiringo, Musoma mjini, ambako mipango ya mazishi inaendelea. Innalillahi 
www.hakileo.blogspot.comwainnailaihirojiun.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company