Tanzania yajibu madai ya News of Rwanda.

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili.
Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda” ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania .
Mahojiano na Salva Rweyemamu
Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale?

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company