SIKU chache baada ya Jeshi la Magereza nchini kukiri mfanyabiashara, Ajay Somai, aliyetupwa jela miaka miwili kwa kosa la kukwapua sh bilioni 3.8 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amepata msamaha wa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Rais Kikwete ana mkono na EPA.Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika eneo la Ifunda, Kijiji cha Mawambala katika Jimbo la Kilolo na Iringa Mjini, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya Operesheni inayoendelea nchi nzima, iliyopewa jina la ‘M4C- Operesheni Pamoja Daima’.
Huku akisikilizwa kwa makini na maelfu ya wananchi wa maeneo hayo, Dk. Slaa alisema ni jambo la kushangaza kwa rais kuwaacha watuhumiwa wadogo kama wale wa wizi wa kuku, lakini ameamua kutoa msamaha kwa wezi wakubwa wa fedha za EPA.
“Hii ni kashfa kwa Rais Kikwete, haiwezekani ukatoa msamaha kwa wezi wakubwa walioiba mabilioni ya fedha halafu ukawaacha watuhumiwa wa makosa madogo, tena wengine wa kubambikiwa kesi na polisi wakiendelea kusota gerezani. Hapa lazima kuna mkono wa Kikwete,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA, alisema kuwa mfungwa huyo wa EPA ambaye yuko nje kwa msamaha wa rais wakati wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikodi ndege kwa ajili ya kampeni za mgombea huyo.
Mbali ya Somai, wezi wengine wa EPA waliopata msamaha huo ni wafungwa namba 24/2011, Farijala Shabani anayetumikia kifungo cha miaka 11 na mfungwa namba 345/2011, Rajabu Maranda anayetumikia kifungo cha miaka kumi, ambao nao wamenufaika na msamaha huo wa rais uliotolewa Desemba 9, mwaka jana.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, CHADEMA ikiingia madarakani wezi hao watakamatwa na kurudishwa gerezani na zaidi ya yote, watalipa fedha walizoziiba.
Mbali na suala la kuachiwa kwa wafungwa wa EPA, Dk. Slaa alisema deni la taifa limezidi kuongezeka ambapo hadi sasa kila Mtanzania hata yule anayezaliwa leo, ana deni la sh 500,000.
Mbowe azidi kulia na Katiba mpya
Wakati Dk. Slaa akirusha kombora kwa Rais Kikwete, Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe, amesema kuwa Katiba Mpya na bora ni ile itakayopata uhalali kutokana na mchakato wake kuhusisha maoni ya watu badala ya masilahi ya chama tawala.
Alisema Katiba ya aina hii ndiyo itasaidia taifa kuponya majeraha na kuondoa makovu ambayo wananchi wameumizwa kwa muda mrefu.
Alisema CHADEMA haitawaangusha Watanzania katika kupigania na kusimamia masuala ya msingi likiwemo suala la Katiba Mpya, huku akiwataka waiunge mkono wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.
Mbowe alisema CHADEMA inatambua umuhimu wa Katiba mpya kwa mustakabali wa Watanzania na jinsi wananchi walivyo na matumaini makubwa kuwa itasaidia kuweka mazingira ya fursa za maendeleo kwa mtu, makundi katika jamii na taifa zima kwa jumla, hivyo watasimama kidete kwa niaba ya Watanzania.
Alisema hayo jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara maeneo ya Muleba, Biharamulo, Chato, Nyang’hwale na Geita, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya operesheni inayoendelea nchi nzima, ikiwa imepewa jina la ‘M4C-Operesheni Pamoja Daima’.
Mbowe ambaye aliingia rasmi kwenye operesheni hiyo tangu Jumamosi wilayani Ngara, alisema kuwa chama chake kwa kuunganisha nguvu za pamoja kwa kushirikiana na kila Mtanzania, makundi mbalimbali katika jamii na vyama vingine vya siasa vilivyo tayari kusimamia mchakato wa Katiba kwa niaba ya Watanzania, kitahakikisha uhai wa Tanzania unapewa kipaumbele kabla ya masilahi ya vyama vya siasa.
“Ndugu zangu wananchi wa Biharamulo juzi nikiwa Ngara nimezungumzia masuala ya Katiba na daftari la wapiga kura, leo pia sina jinsi, nawiwa kuzungumzia suala hili nyeti la Katiba kwenu. Nimesema na nitarudia kusema tena na tena na tena, kwamba suala la Katiba ni uhai wa taifa.
“Kutokana na ukweli huo, kwetu sisi CHADEMA na watu wengine wenye mapenzi mema na nchi yetu vikiwemo vyama vya siasa vilivyo tayari kushirikiana kwa ajili ya jambo hili kubwa linalozidi tofauti zetu zote tunazoweza kuwanazo, tunalichukulia kuwa ni suala la Katiba mpya iliyo bora na inayozingatia matakwa ya Watanzania, ni suala la kufa na kupona.
“Kuna vyama vya siasa vinafikiri katiba zao zinaweza kuwa kubwa kuliko Katiba ya nchi. Tunawataka wafikirie mara mbili sana. Katiba za vyama ni kwa ajili ya vyama hivyo lakini Katiba ya nchi ni kwa ajili ya Watanzania wote nchi nzima. Kuchezea maoni ya watu kwa ajili ya kulinda masilahi ya chama fulani cha siasa ni dharau inayovuka mipaka ya kiburi cha utawala,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Tunataka Katiba mpya hii iende kuponya majeraha na kuondoa makovu ya muda mrefu yaliyoko ndani ya jamii yetu ya Watanzania…wote tumeumizwa kwa namna moja ama nyingine, majeraha na makovu hayo yanaweza kupunguzwa au kumalizwa kabisa na Katiba mpya na bora itakayopata uhalali kutoka kwenu.”