Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kampasi ya Mwalimu Nyerere wakiwa katika jengo la utawala wa chuo hicho.
Na Riziki Mashaka.
Dar es Salaam, kuchelewa kwa mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu hasa katika kampasi ya Mwalimu Nyerere ya chuo kikuu cha Dar es Salaam kumezua hali ya ndivyo sivyo kwani mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliofika chuoni hapo ni ndogo ukilinganisha na idadi yao kamili.
Mpaka sasa wanafunzi wa chuo hicho bado hawajapewa hela zao za kujikimu, hali hiyo imepelekea wanafunzi wengi kutofika katika maeneo ya chuo kwa muda muafaka kwa kuwa wengi wao wanasumbuliwa na tatizo la fedha na matokeo yake kushindwa kumudu baadhi ya mahitaji muhimu, idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hicho hutumia fedha hiyo kujilipia ada na shughuli nyingine za kimaisha kama elimu, maradhi na mambo mengine muhimu hususan ni wale watoto wa wakulima.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa katika Vimbweta katika moja ya eneo maarufu la kujisomea linalojulikana kwa jina la Mdegree.
eneo la jengo la Nkrumah halikuonekana kuwa na watu wengi kama ilivyo kawaida, hii ni kutokana na uchache wa wanafunzi waliofika chuoni hapo mpaka sasa.
idadi ya wanafunzi waliohudhuria katika kampasi ya Mwalimu Nyerere ni ndogo ukilinganisha na idadi kamili ya wanafunzi wa chuo hicho hivyo ofisi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) bado inalifatilia suala hilo kwa makini ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapewa hela zao ili waweze kuendelea na masomo yao.
Baadhi ya wanafunzi wakirudi katika hostel zao za Mabibo hostel.