Helikopta ya CHADEMA yazua gumzo Kalenga



Wananchi wa Kijiji cha Ndiwili mkoani Iringa wakishangilia helikopta iliyombeba mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chadema, Grace Tendega wakati ilipokuwa ikiondoka. Chadema ilifanya kampeni za uchaguzi mdogo kijijini hapo, juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi
Na Geofrey Nyang’oro,Mwananchi
Tukio hilo lilitokea baada ya Chadema kuanza kutumia chopa katika mikutano yake iliyobaki. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, Godbles Lema alisema wanatarajia kufanya mikutano kati ya 76 hadi 100 ndani ya wiki moja.
Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wakazi hao wakiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ndiwili huku baadhi yao wakitumia usafiri wa baiskeli na wengine pikipiki.


Katika mkutano huo, wahutubiaji wakuu walikuwa Wajumbe wa Kamati Ku Chadema Taifa, Godbles Lema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na Mgombea Ubunge, Grace Tendega.


Chopa ya Chadema ilifika katika kijiji hicho saa sita mchana na kufanya mbwembwe kwenye anga la kijiji hicho kabla ya kutua.


Baada ya kutua na wajumbe kupanda jukwaani, viongozi hao waliwashambulia viongozi wa CCM kwa madai kuwa wameanza kuliingiza taifa kwenye mfumo wa kifalme, baada ya kujiwekea utamaduni wa kurithishana madaraka. Akizungumza katika mkutano huo Lema alisema:“Taifa linaelekea kubaya tulipokwenda, na hii inatokana na CCM kuanza mfumo wa kurithishana madaraka,” alisema.


Lema aliwataka wakazi wa Kalenga kuupinga mfumo huo kwa vitendo na kwa kuanza ni vyema wakampigia kura mgombea ubunge kupitia Chadema Grace Tendega.


Naye Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alimshambulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula akidai ni mmoja wa viongozi wasio wakweli kwa wananchi.


Alisema kiongozi huyo aliwadanganya wananchi kuwa chama chake kingewaengue viongozi wote walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa katika kipindi cha miezi sita na hakuna kichofanyika.


“Kama aliwadanya wananchi kuwa angechukua hatua za kuwatimua viongozi wa CCM walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa ndani ya kipindi cha miezi sita na hadi leo hilo halijatekelezeka,atawezaje kuasaidia ninyi wananchi wa Kalenga?alihoji Msigwa na kuongeza;


“Ninaomba msikubali kudanganywa na viongozi hawa alipochaguliwa na kuingia kushika wadhifa w aKaimu mwenyekiti bara alisema anarejesha maadili ndani ya CCM na kwamba angewavua magamba wote walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa ndani ya kipindi cha miezi sita…hadi leo hawajachukua hatua,leo wanawaambia watatekeleza ahadi walizoziahidi zipi walikuw awapi siku zote”alisema.


Msigwa aliwataka wakazi wa Kalenga kutafanya makasa kuchagua CCM kwakuwa viongozi wake hawana dhamira ya kweli ya kuwaaidia wananchi kupiga hatua za maendeleo.


Kwa upande wake Mgombea Ubunge kupitia Chama hicho Grace Tendega aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo wakazi wa Jimbo la Kalenga.









Alisema mara atakapochaguliwa atahakikisha anafunga vizuizivya mazao vilivyowekwa barabarani kwa ajili ya kuzuia wananchi kwenda kuuza mazao yao nchi ya vijiji vyao.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company