Dar es Salaam. Chadema imekosoa uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick kuzuia waendesha bodaboda, bajaji na maguta wasifike Posta kwa kile walichodai kuwa hakufuata kanuni.
Akizungumza jana, Dk. Wilbrod Slaa alisema uamuzi huo aliuita ni batili kwa kuwa alitakiwa kukaa mezani na viongozi wanaoendesha usafiri huo na siyo kutoa kauli yake kwenye vyombo vya habari bila ya kuwashirikisha wao.
Dk. Slaa alisema Serikali ilitakiwa kukaa na viongozi nao chini ili waweze kutoa mawazo yao ambayo yangeweza kuleta mwafaka.
“Kilichotokea mkuu wa mkoa huyo alitangaza kuwa vyombo vya usafiri wa bodaboda, maguta na bajaji zisifike Posta, badala yake kila dereva aishie kwenye wilaya yake na hakuna barua ya maandishi walioandikiwa hii ni batili,” alisema Dk. Slaa.
“Hivyo nimeongea na mkuu wa mkoa ameniambia kuwa kesho atakutana na viongozi wenu ili muweze kufikia mwafaka wenu na nina imani mtaelewana endapo mtashindikana nawaomba mrudi kwetu ili tujadiliane,”alisema Dk. Slaa.
Alisema haingii akilini kuona Serikali inachukua kodi kutoka kwao. Hivyo wanatakiwa wawaachie waendelee kufanya biashara hiyo hadi hapo mwafaka wao utakapopatikana.
“Hivyo kama Serikali inaamini kuna utawala bora, naamini watawaachia wale wote waliokamatwa kutokana na makosa ya kufika posta,” alisema.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago