Kupatikana kwa ndege ya Malysia iliyopotea imekua kama ndoto


Juhudi za kuitafuta ndege aina ya MH 370 ya Malaysia Airlines zinaendelea.
REUTERS/Kham   Na RFI
Meli ya Marekani ambayo imekuwa ikishiriki katika juhudi za kimataifa za kutafuta ndege ya Malaysia iliyopotea inatazamiwa kuondoka na kurejeshwa Marekani licha ya kuwa juhudi hizo hazijakamilika. Maafisa wa ngome kuu ya jeshi la Marekani wamebainisha.
Juhudi za kimataifa za kutafuta ndege hiyo zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo, huku wakichambua maneno ya mwisho aliyoyazungumza rubani msaidizi kabla ndege hiyo kutoweka.

Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama ''Kila kitu ni shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rada kuzimwa.

Awali rais wa tume ya bunge inayohusika na usalama wa ndani nchini Marekani, Michael McCaul, alifahamisha kwamba ndege hio ya kampuni ya Malaysia Airlines iliyopotea tangu juma moja iliyopita, huenda ilitekwa na kufichwa sehemu moja ili itumiwe katika mshambulizi ya kigaidi, kama yale yaliyotokea nchini Marekani septemba 11.

Akihojiwa kwenye kituo cha televisheni cha Fox News, McCaul alibaini kwamba kwa sasa, hana imani kwamba kupotea kwa ndege hio kunahusiana na vitendo vya ugaidi, lakini kwa mujibu wa mjumbe huyo, viongozi wa Marekani wana imani kwamba ndege hio ilitua sehemu moja ili iweze kutumia katika mashambulizi mengine.

Ndege hio ilichukua njia mbili, baada ya kupoteza mawasiliano: huenda ilielekeza kaskazini chini Kazakhstan, hata hivyo,ingeliweza kugunduliwa na rada.

“Uwezekano mwengini ni kwamb, huenda ndege hio ilitua katika nchi ya Indonesia, na huenda ikatumia katika mashambulizai ya kigaidi, kama ilivyokuwa septemba 11”, amesema Michel McCaul.

“Lakini ukweli tu ni kwamba, ndege hio haikufanya ajali. Ni kitendo kiovu kilichodhamiriwa, swali ni kujua nani anaye husika na kitendo hicho” amesema McCaul.
Mataifa ishirini na tano yanashiriki katika kuitafuta ndege hio iliyopotea, ambayo ilikua na abiria 239.

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company