Ufisadi nchini Kenya umechangia pakubwa maisha duni miongoni mwa wananchi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanzisha rasmi mpango maalum wa tume ya maadili na kupambana na rushwa unaolenga kukabiliana na tatizo hilo.
Mpango huu unazinduliwa wakati Kenya ikikabiliwa na kashfa mbali mbali za ufisadi .
Rais Kenyatta ameamrisha ofisi ya mkuu wa sheria, idara inayohusika na masuala ya haki na fedha pamoja na tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya kubuni sera zitakazosaidia katika harakati za kupiga vita ulaji rushwa.
Sera hizo ambazo ripoti yake inalenga kutolewa mwisho mwa mwaka huu zinanuia kuimarisha vita dhidi ya ufisadi mashinani .
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mpango wa miaka mitano wa tume ya kupambana na rushwa nchini Kenya rais Kenyatta amesema kuwa viwango vya sasa vya rushwaa vinahitaji mipangilio bora ya sera ili kuvipunguza.
Rais Kenyatta amesema kuwa ni jambo linalokubalika kuwa ili kushinda vita dhidi ya ufisadi ni lazima kuwa jamii ikubali kuwa uwe mpangilo wa kudumu na ni sharti wakenya wabadili mienendo yao," ni lazima tujenge na kukuza jamii inayozingatia uwzi na haki kama nguzo ya taifa." alisema rais Kenyatta.
Wakati huo huo rais Kenyatta ametoa amri kwa mkuu wa sheria,idara ya haki , wizara ya fedha tume hiyo ya kupambana na ufisadi kuharakisha mpango wa kubuni sera hizo ili kufanikisha mpango wa serikali wa kutokomeza ufisadi.