Obama aionya Urusi kwa vikwazo zaidi

Rais Obama yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.

Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama Marekani na Ulaya
Kwenye hotuba muhimu kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.

Akizungumza mjini the Hague kabla ya kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.

Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi. Amesema japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio itakayoathirika zaidi.

Mkutano huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company