Raia waandamana dhidi ya Umoja wa Mataifa-Juba


Raia wa Sudan Kusini wakiandamana
Zaidi wa raia elfu moja wa Sudan Kusini, wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba, dhidi ya Umoja wa Mataifa, wakiishutumu kwa kuwapa waasi wanaopambana na serikali silaha.

Waandamanaji hai wamemtaka mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilda Johnson kujiuzulu.Siku ya Ijumaa, serikali ya Sudan Kusini, ilisema kuwa ilinasa msafara wa magari yaliyokuwa yakisafirisha silaha ambazo huku zikidai kuwa zilikuwa zikisafirisha misaada ya chakula.

Umoja wa Mataifa umekanusha shutuma hizo, lakini imekiri kuwa imekiuka mkataba waliosaini na serikali ya nchi hiyo, kwa kusafirisha silaha wakitumia magari badala ya ndege.

Taifa la Sudan Kusini, limekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu Desemba mwaka uliopita, wakati wanajeshi watiifu kwa makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Riek Machar, kuanzisha mapigano katika kambi kuu ya jeshi mjini Juba.

Mazungumzo ya amani kati ya wawakilishi wa serikali ya Sudan Kusini inayoongozwa na Salva Kirr na makamu wake wa zamani Riek Machar, yanaendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company