Rais Olexandre Tourtchinov haikubaliane na madai ya kujitenga kwa eneo la Crimea na Ukraine


Rais wa mpito wa Ukraine, Olexandre Tourtchinov.
AFP / SERGEI SUPINSKY  Na RFI
Rais wa kipindi cha mpito nchini Ukraine Olexandre Tourtchinov amesema nchi yake haiwezi kufuata mchezo unaochezwa na Urusi kwa kutaka eneo la Crimea kujitenga na Ukraine na kwamba hawawezi kuingilia kijeshi mzozo huo badala yake wataulinda mpaka wao wa eneo la mashariki.Akizungumza katika kikao cha kitafa cha baraza la usalama wa ndani, rais Tourtchinov amepinga vikali kura ya maoni inayo tarajiwa kuitishwa jumapili hii na viongozi wa Crimea kutaka kujitenga na ukraine na kudai kuwa mipango yote inaandaliwa katika ofisi za Ikulu ya rais nchini Urusi Kremlin.

Maandamano yameshuhudiwa juma lililopita katika eneo la Donetsk na Lugansk ya watu wanaotaka mjitengo wa eneo la Crimea na Ukraine ambapo ofisi za taasisi tawala zilivamiwa na waandamanaji hao huku bendera ya Ukraine ikipandishwa.

Waziri mkuu wa Ukraine Arsene Iatseniouk anataraji kupokelewa alhamisi hii kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN, ambapo atawasilisha taarifa kuhusu hali halisi nchini Ukraine na katika eneo la Crimea linalo taka kujitenga.

“Hatuwezi kuingilia kijeshi mzozo unaoendelea katika eneo la Crimea, badala yake tutaulinda mpaka wetu wa eneo la mashariki, na iwapo Ukraine haitolindwa, jeshi la urusi huenda likaingilia kijeshi taifa letu kwa faida ya taifa lao”, amesema Tourtchinov, ambae ni mkuu wa majeshi ya Ukraine wakati akihojiwa bungeni baada ya kuendesha mkutano wa baraza la usalama lakitaifa na ulinzi, huku akibaini kwamba idadi kubwa ya wanajeshi na vifaru wametumwa kwenye mpaka ulioko mashariki mwa Ukraine.

Tourtchinov ameinyoshea Urusi kidole cha lawama kwamba imekataa wito ambao umekua ukitolewa na Jumuiya ya Kimataifa wa “ kuiomba Urusi kuanzisha mazungumza ya amani”.

Tourtchinov amepongeza mataifa ya magharibi kuonesha uungwaji wao mkono kwa utawala wa Ukraine na kuitaka Urusi iachane na uchokozi.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Ukraine, Arseni Iatseniouk, yuko njiani akielekea Marekani kukutana na hio kesho na raisa Barack Obama.

Hayo yakijiri, taasisi mbili za bunge na baraza la seneti wameidhinisha jana waraka unaolani uingiliaji usio halali wa Urusi nchini Ukraine.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company