Waziri huyo wa uchukuzi Hishammuddin Hussein aliwaambia waandishi habari Jumapili kuwa idara za kijasusi za Malaysia zinapeleleza orodha ya abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo na kushirikiana na wenzao wa kimataifa ikiwemo idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya Marekani FBI.
Maafisa wanasema pia kuwa kifaa cha ufuatiliaji wa safari za ndege kinaashiria ndege hiyo ilirudi nyuma badala ya kuendelea na safari yake kabla ya kutoweka. Timu za uokozi bado zinaendelea na juhudi za kuitafuta ndege hiyo.